MBINU ZA KUZINGATIA KATIKA UANDAAJI WA CHAKULA KWA KUKU WAKO

1.   MAJI

Maji ni muhimu sana kwa kuku wawapo bandani. Wape maji ya kutosha kila wakati unapoona yanapungua/kuisha ili waendelee kuyeyusha chakula wanachokula Nna kupunguza joto mwilini. Kuku 1 anaweza kunywa hadi robo lita ya maji kwa siku. Kwa hiyo utawawekea kulingana na wingi wao. Pata chombo kizuri ili uwaning’inizie juu kidogo kutoka usawa wa ardhi. Hii itasaidia kupunguza uchafuzi wa maji na magonjwa yanayoenezwa kwa njia ya maji. 

Hakikisha kuwa maji ni safi na salama.
2.    CHAKULA.
Ni vema kutafuta vifaa vizuri kwaajili ya kuwawekea chakula. Tafuta vyombo ambavyo utaweza kuning’iniza/tundika juu kidogo kutoka chini kulingana na umri wa kuku. Hii itasadia sana kupunguza uwezekano wa kutosambaa kwa magonjwa hasa yale yanayoenezwa kupitia viatu tunvyo vaa tunapoingia bandani. Pia itasaidi sana kupunguza chakula kinacho mwagika chini wakati kuku wanapokula.
Kwa mfugaji yeyote wa kuku anapaswa kuelewa kuwa chakula cha kuku ni ghali. Hivyo ni vema kufuata taratibu vizuri katika ulishaji na kutengeneza/kununua vyombo ambavyo kuku hataweza kumwaga chakula. Kumbuka kwamba kama vyombo siyo vizuri basi vitamwaga chakula kingi na hivyo kukuletea hasara.
Ili kuweza kupata mazao mazuri yenye faida, ni vema ununue chakula cha kuku madukani au utengeneze wewe mwenyewe kama nitakavyoeleza hapa chini ili uwape kuku wako chakula chenye viini lishe vyote muhimu kwa kuzingatia umri wa kuku ulionao. Kwa vifaranga, unaweza kuwawekea chakula chini kwenye magazeti/mifuniko ya ndoo/sahani. Baada ya siku 10 unaweza kuwawekea kwenye chombo maalum.

Namna ya kuandaa chakula cha kuku.
Vyakula vya kuku vinapaswa kuwa na aina/viini lishe muhimu kama vile Protini, Wanga, madini na Vitamini.
Vyakula hivyo vimegawanyika kama ifuatavyo;· Vyakula vya kujenga mwili ni; Jamii ya kunde,samaki, dagaa,mashudu ya ufuta/alizeti/pamba,· Vyakula vya kulinda mwili ili usipatwe na maradhi ni; Mafuta ya samaki na majani mabichi kama vile; kabichi, mchicha,majani ya mpapai na nyasi mbichi.· Vyakula vinavyojenga mwili/mifupa ni kama vile; Aina za madini, chokaa, chumvi na mifupa iliyosagwa.· Vyakula vilivyotajwa vinaweza kumkuza vizuri kuku hadi uuzwaji/kuliwa kwake. Surghum Larrymeal huzuia kudonoana, huboresha kiini cha yai na kuongeza mayai. Changanya kg 1 kwa kg 50 za pumba.

PITIA
UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA [ BROILER ]

Ukosefu wa madini kama fosforasi na kalsiam husababisha matege, vidole kukunjamana, kufyatuka kwa misuli ya magoti, kuwa kilema na kupofuka macho kwa kuku.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

KILIMO CHA UYOGA

Kwa kuwa #uyoga upo wa aina mbalimbali, usitawishaji wake hutofautiana katika mahitaji yake, ikiwa ni pamoja na hali ya hewa, malighafi za #kuoteshea, urahisi wa

Read More »
Bata Dume

UFUGAJI BORA WA BATA

UFUGAJI BORA WA BATA : Wafugaji wengi wadogo wa bata hapa nchini hufuga bata machotara ambao wamechanganyika damu aina mbalimbali. Matumizi makubwa ya bata hawa

Read More »

FAIDA ZA MBOLEA YA MBOJI

Matumizi ya mbolea ya mboji katika kilimo cha mazao yana faida zifuatazo; Utengenezaji wa mbolea ya mboji hauna gharama na ni rahisi hivyo wakulima wa ngazi

Read More »
Udongo

Njia sahihi za kilimo bora

Njia sahihi za kilimo chochote kile ambacho unatamani sana kukifanya zipo kanuni na taratibu zake za kuweza kufanya hivyo. Baadhi ya mambo ya msingi ambayo

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »