MFAHAMU MDUDU HUYU MWARIBIFU WA MAHARAGE KWA UNDANI ZAIDI

Funza wa vitumba ni nondo, na ni mdudu mharibifu maarufu wa kunde na maharage mengine kote Afrika Mashariki na Magharibi. Viwavi hula vitumba na maua, na kuingia ndani ya mifuko ya maharage na kuacha tundu kwenye mfuko wa maharage na kula mbegu.

Je huyu mdudu yukoje?Nondo aliyekomaa hutaga mayai moja moja au katika makundi madogo juu ya maua au vikonyo vya maua na pia kwenye vichomozo vya mimea michanga. Mayai yana umbo la mduara dufu, rangi nyeupe na manjano nyepesi; yai moja linaonekana kama tone dogo la maji. Larvae, au viwavi, vinaweza kukua na kufikia urefu wa milimita 17-20.
Viwavi huwa rangi ya kijani chepesi na madoa ya kahawia-meusi na kichwa ni rangi ya kahawia iliyokolea. Viwavi wachanga hupatikana katika makundi wanapokuwa katika hatua hii, lakini baadaye kupatikana kila mmoja kivyake. Viwavi wachanga hushambulia maua na majani, lakini viwavi waliozeeka wana uwezo zaidi wa kutembea na mara nyingi wanapatikana wakila na kutoboa na kuingia ndani ya mfuko wa mbegu ambapo hula mbegu zinazokua. Vinapokomaa viwavi huanguka kutoka kwa mmea mpaka mchangani ambapo hubadilika na kuwa pupa wakiwa chini ya takataka.

Kiwavi wa nondo akiwa ndani ya jumba la maharage (podo)
Mbawa za nondo ni nyeusi-kahawia na zina alama nyeupe juu ya mbawa za mbele na upana wa mbawa wa milimita 20-25. Nondo huchangamka usiku. Wakati wa mchana hupatikana wakipumzika upande wa chini wa majani na mbawa zao zikiwa zimetandazwa.
Kuna hatua nne katika mzunguko wa maisha: mayai, viwavi, pupae na nondo aliyekomaa. Kukua kwa mayai huchukua wastani wa siku 3, hatua ya viwavi huchukua wastani wa siku 13-14, hatua ya pupae siku 6-7 na nondo waliokomaa wanaweza kuishi kwa wastani wa siku 6-10.
Maharage yanashambuliwa yakiwa katika hatua gani?Maharage hushambuliwa na funza wa vitumba kuanzia wakati wa kutoa vitumba mpaka wakati wa kuvuna. Angalia matundu ya mviringo kwenye maua na pia majani yaliyokunjwa ambayo yamekwama pamoja. Fungua maua na uangalie viwavi. Mifuko ya mbegu itakuwa na tundu la wazi ambalo kiwavi aliingilia. Angalia mipira ya manjanokahawia nje ya mifuko ya mbegu; hiki ndicho kinyesi kilichoachwa na viwavi walipoingia ndani ya mfuko wa mbegu.

PITIA
Kwa nini Upunguze kuku wako midomo?

Njia Za Kudhibiti Funza Wa Vitumba
Kinga – mambo ya kufanya kabla dalili kuonekana
Mbinu za kitamaduni: Panda mapema ili kuepuka kipindi cha ushambulizi mzito.Tumia aina sugu / zakuhimili na /au za kukomaa mapema ikiwa zinapatikana katika eneo lako.Ondoa mimea mingine wenyeji kama vile maharage ya kawaida, kudzu, maharage ya lima, pojo na mimea mingine ya mikunde kutoka ndani na nje ya shamba.Kupanda mseto maharage na mtama au mahindi kunapunguza idadi ya wadudu wakutoboa mifuko ya mbegu na kupunguza hasara ya mavuno.Fanya mzunguko wa maharage na mahindi.

Kudhibiti – mambo ya kufanya baada ya dalili kuonekana
Mbinu za kitamaduni: Okota kwa mkono mayai na viwavi kutoka kwa mimea na uviharibu.Kata majani yaliyofungwa fungwa pamoja yenye nyuzi nyeupe za hariri na pia uondoe majani yaliyozeeka ili kuruhusu mwanga zaidi kufikia majani na mashina ya mimea.
Mbinu za kikemikali: Ni vigumu kudhibiti funza wa vitumba na dawa za kuua wadudu kwa sababu hubaki wamejificha ndani ya mfuko wa mbegu / maharage.Dawa ambazo unaweza kutumia kuua hawa wadudu ni pamoja na Thiodan, dusban, serecron and Kar

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

KILIMO BORA CHA MPUNGA

Mpunga ni kati ya mazao ambayo yanalimwa sana dunian na pia ni kati ya mazao ambayo yanapendwa sana na watu kutokana na chakula chake juwa

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »