FAIDA ZA MIPARACHICHI, MIEMBE NA MICHUNGWA

Share on facebook
Share on whatsapp
Share on twitter
Share on telegram
Soma kwa umakini itakuchukua dakika chini ya Kumi......
Miparachichi

1.1 MIPARACHICHI

 

Miparachichi imekuwepo nchini kwa miaka mingi. Katika mikoa ya kaskazini (Kilimanjaro na Arusha) pamoja na kutumika kama matunda, maparachichi yalibeba jina la chakula cha mbwa kwa kuwa mara nyingi yalipodondoka kutoka kwenye miti yaliliwa na mbwa. Hata hivyo, mikoa ya kusini (Mbeya) maparachichi yamekuwa tunda muhimu katika milo yote.

Utafiti umeonesha kwamba maparachichi yana mafuta muhimu yanayoondoa mafuta yanayoganda kwenye mishipa ya damu. Pia yana virutubisho vinavyofanya damu itembee kwa urahisi mwilini. Maparachichi yana virutubisho vya vitamini E. Kwa sababu hii maparachichiyanatumika katika kutengeneza vipodozi ya ngozi na nywele.
Matunda ya parachichi yanaweza kuliwa kwa namna tofauti. Yanaweza kuliwa kama kituliza njaa wakati ukisubiri chakula kingine au kilainisha chakula baada ya mlo. Pia parachichi linaweza kuliwa sambamba na chakula kingine kwa mfano ndizi za kuchoma. Maparachichi yanatumika pia kutengeneza juisi.
Matunda machanga yaliyoanguka yanatumika kuharakisha uivishaji wa ndizi kwa kuzifanya ndizi ziive zote kwa pamoja.
Majani ya miparachichi yanatumika kulishia mifugo kama mbuzi na ngombe wakati miti yake inatoa mbao nzuri za kutengenezea samani.
Hivyo miparachichi inaweza kuwa chanzo kizuri cha pesa kwa familia na wajasiliamali soko lake likiboreshwa.
Miparachichi huweza kustawi sehemu nyingi zenye hali ya hewa ya kitropiki iliyo na kipindi cha ubaridi, joto kiasi na mvua za kutosha.
Hivyo, hapa nchini kilimo chake kimeshamiri zaidi kwenye maeneo ya nyanda za juu mikoa ya Mbeya, Iringa, Morogoro, Kilimajaro na Arusha. Sehemu nyingine zilizo kwenye miinuko mfano Lushoto mkoani
Tanga zao hili laweza kulimwa. Hata hivyo kulingana na aina ya miparachichi, maeneo ya nyanda za chini yasiyo na vipindi virefu vya ukame yanaweza pia kustawisha zao hili. Kwa vile miparachi ni miti inayo kua haraka na haipukutishi majani, hivyo ni mti mzuri katika kuhifadhi mazingira.
Endapo miti hii itapandwa kwa wingi itakuwa ni kivuto cha ukusanyaji wa hewa ya ukaa inayotokana na ongezeko la mabadiliko ya tabia nchi.

PITIA
CHAKULA BORA CHA SUNGURA - Jifunze Maarifa ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi

1.2 MIEMBE

miembe

Embe ni tunda maarufu na limekuwa likitambulika kama mfalme wa matunda. Matunda ya embe yanatumika yakiwa mabichi au yameiva. Matunda yaliyoiva yanaliwa kama tunda au pia yanaweza kutengenezwa juisi na jam.
Embe mbichi hutumika katika kutengeneza achali. Kama ilivyo kwa miparachichi, miembe hukua haraka na haipukutishi majani na hivyo ni mti unaobadilisha mazingira ya mashamba na kuleta hali ya ukijani kwa mwaka mzima.
Miti ya miembe ikipandwa kwa mpango mzuri mashambani inasaidia kurekebisha hali ya hewa kwa kupunguza joto, kuvuta mawingu ya mvua, kupunguza kasi ya upepo, kupunguza mmomonyoko wa ardhi na kufyonza hewa ya ukaa.
Hivyo Miembe nayo ni miti mizuri kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Miti hii ikipandwa mashambani kwa mpangilio mzuri wakulima wataweza kulima mazao menginena hivyo kujipatia fedha zaidi, matunda na hata kuni.
Miembe hustawi sehemu zenye joto la wastani na lenye maji au mvua za kutosha, hata hivyo miembe haistawi vizuri katika maeneo yenye baridi kali na mvua nyingi kwa mwaka kwa kuwa inahitaji kipindi cha ukame cha miezi isiyopungua miwili hadi mitatu ili kuwezesha kutoa maua. Pia miembe hihutaji udongo wenye kina usio twamisha maji na usio na chumvi chumvi.

1.3 MICHUNGWAMichungwa

Michungwa pamoja na aina ya matunda yaliyo kwenye jamii yake kama vile machenza, madaransi, mapomelo, malimau, ndimu n.k. pia ni matunda maarufu katika sehemu za nchi za joto na zile za joto kiasi.
Matunda haya hutumika mara nyingi yakiwa yameiva kwa kuyala moja kwa moja au kutengeneza juisi na jam.
Yana vitamini C nyingi pamoja virutubisho vingine vinavyohitajika kwa mwanadamu.
Machungwa pamoja na jamii yake huwapa wakulima faida wakati wa mauzo na pia huongeza thamani ya mashamba yao. Wadau wengi hunufaika kutokana na kilimo cha matunda haya. Kwa mfano walanguzi na wafanya biashara wengine kama wale wasafirishaji hujipatia faida.
Miti ya michungwa kama ilivyo kwa miti mingine, kutumia hewa ya ukaa na hutengeneza kivuli na hivyo kupoza joto.
Michungwa huweza kustawi kutoka ukanda wa pwani hadi sehemu za miinuko ya kiasi cha mita 2000 kutoka usawa wa bahari. Pia miembe hihutaji udongo wenye kina usio twamisha maji na usio na chumvi chumvi.
Machungwa pia huhitaji kipindi kifupi cha ukame ambapo baada ya kupata maji hutoa maua.

PITIA
UFUGAJI WA KUKU BORA WA NYAMA (BROILER) HATUA KWA HATUA

 

source:kilimobiashara.net

Diana Mussa

Diana Mussa

Mwana Blogger mahiri,aliyehama fani yake kutoka kwenye urembo na mitindo hadi kwenye uwanda wa kilimo ,na kuitumia sekta hii ya kilimo kwa kutoa taarifa zilizo sheheni mambo tele ~ na kushare kwa Watanzania,katika ulimwengu huu wa Teknolojia

Leave a Reply {Acha Maoni yako hapa}

Kuhusu Sisi

KilimoTanzania tumejikita kukupa Elimu pekee ya Kilimo kwa Gharama sawa na Bure, Ili tuweze kuwa na Taifa bora lenye wajisiriamali katika sekta ya kilimo na Ufugaji.

Kwa Mawasiliano usisite Kubonyeza hapa 

Vitabu Vya Kilimo na Ufugaji pia vinapatikana  Kwe Ukurasa Huu

Jiunge channel Yetu ya Telegram

Karibu uweze Kujiunga na Channel Yetu ya Telegram uwe wa Kwanza kupata ,Taarifa moya za kuhusu Kilimo mara zinapowekwa kwenye Tovuti Yetu

Nyaraka Mpya

Follow Us

Video Mbali mbali za Kilimo