MISINGI YA KILIMO BORA CHA DENGU

Dengu ni nafaka kama zilivyo nafaka zingine, ni zao la jamii ya mikunde pia ni zao la biashara, ni miogoni Mwa zao muhimu sana la biashara ukanda wa ziwa kwa sababu ya thamani yake Kuwa juu sana, zao hili hutumika pia kama zao la chakula kama mbonga , mchaganyo wa wali mseto , makande , kutegeneza Bagia , chiichiri namengineyo mengi.

Kanda ya ziwa hili ndiyo Zao llinalotegenewa zaidi likiogozwa na zao la choroko kwa kuwa na thamani kubwa, hivyo zao hili nizao muhimu kwa uchumi wa wanakanda ya ziwa.Dengu ni zao la chakula na biashara lenye kiasi kikubwa cha protini, vitamini A na B, Madini ya Potassium na chuma. Zao hili likilimwa vizuri linaweza kutoa mavuno ya kilogram 200 hadi 500 kwa ekari. Zao hili huchukua wastani wa siku135 kupandwa hadi kuvunwa.

HATUA MUHIMU KATIKA KILIMO CHAKEKilimo cha ndegu ni kilimo rahisi sana hakina usubufu sana kama yalivyo mazao mengine hasa ukifata utaratibu wa hatua za mwanzo.

Mambo ya kuzingatia1. Kuwa makini na hali ya hewa ya mwaka husika kwa kuangalia ukame katika mbuga utaaisha lini pia hali ya mvua ikoje kwa maana kuwa msimu wa kulima huwa mwezi wa tatu mwishoni kwenye maeneo ambayo mbuga huwahi kukauka mapema yaani muda huo ndiyo watu huanza kuandaa shamba kwa kulilima mara ya kwanza kama hatua ya kukiandaa shamba pia hatua hii hufanyika mwenzi nne lakini iwe kwenye kumbukumbu sahihi kuwa ndegu kwa hali ya uzuri kabisa hulimwa mwezi nne na mwanzoni kabisa mwa mwezi wa tano kabla mbuga hazichakauka .
 2. Uchaguzi wa Mbengu, mbengu bora za dengu ni muhimu kuzifahamu na kuzitumia katika kilimo hiki  Ziko mbengu ambazo hazihimili magonjwa lakini zipo zinazohimili magonjwa na zinakuwa na uzito hii husaidia katika swala la uuzaji kwa maana ya kuwa mara nyungi dengu kwa sasa huuzwa kwa kilo ili mkulima apate faida zaidi

3. Baada ya kulima mara ya kwanza kama kuliandaa shamba unapaswa kulima mara ya pili na kupanda mbengu kwa kufata misitari au kufata tumba au vitalu au misingi itakayokuwa imeadaliwa.

PITIA
Jifunze kanuni za kilimo bora cha Rozela

4. Hakikisha dengu unapanda katika mbunga isiyo na maji yaliyotuama , unyevunyevu  wa udogo wa shambani ndiyo hitaji muhimu la uoteshaji dengu hairuhusiwi kabisa kupanda dengu kwenye shamba lenye maji.5. Ardhi inayofaa kwenye kilimo cha dengu ni shamba nyeusi au udongo mweusi ambao hutumika pia katika kilimo cha mpunga, mahidi, choroko na mengineyo .

6. Baada ya dengu kuota hakijisha hakuna maji yaliyotwama katika shamba lako

7. katika ulimaji wa dengu palizi haina ulazima mara nyingi dengu haina palizi kabisa ukizigatia hatua za mwanzo za uandaaji wa shamba

8. Dengu hutumia miezi mitatu mpaka kuvuna hivyo inajulazimu kusubiri ikauke mpaka hali ujano itokee kwenye mmea, mavuno ya dengu mara zato hufanyika kwa kung’oa mmea wote na kukusanya sample dogodogo ili kumaliza mapema mavuno yake baada ya hatua hiyo unaleta mkokoteni shambani unajusanya kwa mkokoteni nakupeleka sehemu kavu iliyosafi kwa ajili ya kutoa maganda ya zao la dengu,hatua ya kutoa maganda ya dengu inaweza fanyika kwa kienyeji kwa kupiga na miti au ikatumika kwa kitaalamu kwa kupiga .
na Tractor yaan tractor inapita kwa mzuguko kwenye navuno ya dengu yaliyosambazwa mpaka kuputua maganda ya juu ya dengu na kubaki dengu yenyewe tayari kwa biashara au kukoborewa tena kwa chakula.

9. Uhifadhi wa zao la dengu hauna chagamoto sana japo hushambuliwa na wadudu baada ya miezi mitatu bila kuweka dawa unapaswa kuhifadhi kwenye eneo la wazi yaan kama ni chumba kiwe na uwazi wa hewa ya kutosha  lakini pia kunagunia special nitazieleza kwenye utatuzi wa chagamoto.


CHAGAMOTO KATIKA KILIMO CHA DENGU


Zipo chagamoto kadhaa katika kilimo cha dengu kama ifatavyo1. Wakati wa kupanda huwa kunachagamoto ya mvua ambazo hujitokeza na kuharibu zao la dengu kwa kisukuma tunaita SHIBOJA yaani mvua za kuozesha dengu chagamoto hiyo ikijitokeza subiri maji yakauke katia mbengu upya kama zao limeathiriwa kidogo kama limeathiriwa sana unarudia shamba lote.

PITIA
KAZI YA KILIMO TANZANIA.

2 Chagamoto ya Funza baada ya mmea kutoa maua . mmea ukitoa maua funza hushambulia kwa kasi kama eneo hilo liko na funza tiba ya funza hao nikupulizia dawa unaenda duka la kilimo watakupatia.

3 chagamoto ya wadudu wakati wakati mmea unatoa zao lenyewe Wakati huu pia unapulizizia dawa kama wakijitokeza Jambo la funza na wadudu hujitokeza mara chache sana hivyo ni vyema kuwa na.tahadhali hiyo.

4 Chagamoto ya panya Panya hujitokeza kwenye shamba wakati zao Linaanza kukomaa wao hutafuna dengu kamili hivyo unaweza jikuta unapata hasara wakati dengu zilisitawi vyema, Utatuzi wa chagamoto hiyo ni kuwatega panya kwa sumu kwa ukanda wa mkoa wa shinyanga serikali hutoa dawa nasi huchaganya na mahidi nakusambaza pembezoni mwa shamba maana panya hutokea kwenye nyasi hivyo watakutana na mahidi nakuyala.

Chagamoto nyingine ni za masika unaweza lima mwishoni sana kwenye mavuno ukakutana na mvua.5 Chagamoto ya uhifadh Hapo kunachagamoto ya kushambuliwa na wadudu ndani ya miezi mitatu ya mwanzo unashauriwa kuhifadhi kwenye magunia nasiyo mifuko ya plastic.

Unashauriwa kutia dawa inaitwa AKTERIA mapema kabisa unapohifadhi kama unahifadhi kwa muda mrefu baada ya miezi mitatu unatia tena Au unaweza hifadhi kwaifuko maalumu ambayo imetiwa dawa kabisa na dani inajuwa kama mfuko wa sukari na upaswa kuifuga kitaalamu kama maeelekezo yalivyo .Chagamoto nyingine ni ya soko naieleza hapa chini na utatuzi wake

HALI YA HEWA NA UDONGO Ni zao linalohitaji hali ya hewa ya kibaridi kiasi kwani joto kali na ukame sana huathiri mavuno yake, hupunguza wingi wa mavuno. Ni zao linalostahimili ukame, linaweza kukua katika hali ya hewa ya unyevunyevu tu.

Kama utakuwa unamwagilia basi epusha unyevu mwingi ikifikia kipindi cha maua hadi kuvuna. Zao hili linaweza kulimwa katika udongo wa aina tofauti tofauti wenye Ph 6-8. Udongo wenye asidi na base kidogo.Kwa Tanzania zao hili linaweza kulimwa katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Mwanza, Singida, Morogoro, Shinyanga N.K. Lakini kwa sasa mikoa yaShinyanga na Mwanza ndio wazalishaji wakubwa wa Dengu.


UPANDAJI NA NAFASI Zao hili huitaji mbegu kiasi cha kilogram15 hadi 40 kutegemea ukubwa wa mbegu husika. Zao hili hupandwa mwishoni mwa msimu wa mvua,unaweza kupanda baada ya kuvuna mazao mengine uliyopanda mapema.
Mbegu za dengu hufukiwa katika kina cha sentimeta 5 hadi 6 ili kufanya mazingira rafiki kwa bacteria wa rhizobia kufanya kazi. Zao hili usipande pamoja na vitunguu na tangawizi. Panda kwa kutumia drilling method-njia ya vifereji kwa nafasi ya mistari miwili ya sentimeta 15 na sentimeta 30 hadi 50 kwa mstari hadi mstari.


MBOLEA ZA VIWANDANI NA SAMADIMbegu unaweza kuzipanda baada ya kuziongeza inoculam kundi F na Pia Mbolea ya DAP kilogram 25 hadi 50 kwa ekari katika shamba lisilo na rutuba ya kutosha.

PITIA
FAIDA ZA UTUMIAJI SAMADI MASHAMBANI

PALIZI-Palilia mapema shamba lako.

WADUDU WAHARIBIFU KWA DENGUDengu hushambuliwa na Mchwa wakubwa weusi, aphid wa njegere, funza wa vitumba, Inzi wa lucina n.k. wazuie wadudu hawa kwa kupuliza dawa za wadudu mara tu uonapo dalili za mashambulizi ya wadudu.

MAGONJWA YA DENGUDengu hushambuliwa sana na magonjwa ya ukungu ambayo. Hivyo kama eneo lako hushambuliwa na ukungu mara kwa mara basi puliza dawa za ukungu (FUNGICIDES ).

UVUNAJI WA DENGUZinavunwa mara tuu pindi vitumba vya chini vibadilikapo rangi kuwa kahawia angavu na vitumba vikiguswa hutoa sauti Mavuno ya dengu kwa heka yanaweza kuwa gunia 6,5,4 Inategemeana na eneo ulilolima linarutuba kiasi ngani na umefata taratibu zote.

Soko la dengu ni la uhakika sana kwa maana ya uhitaji wa dengu katika soko la ndani na nje
Dengu ndiyo zao ambalo mkulima wa mkoa wa shinyanga na niko jirani hulitegemea kwa kipato cha juu.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

HIZI NDIZO TOFAUTI YA ASALI YA NYUKI WADOGO NA ASALI YA NYUKI WAKUBWA

Watuwengihuwatunatumiaasalipasipokujuawametokananaasaliwaainagani, hivyokilaasaliambayounaitumiakuanzialeonilazimaujuewanatakonananyukiwaainagani. AsalizaNYUKI WAKUBWA na WADOGO zinatofautianakatika mambo kadhaanahvyonimuhimukujuatofautihizokablahujanunuailikuanauhakika. NYUKI WADOGO 1. Ni nyepesizaidikwaniinakiwango cha majikuanziaasilimia 24 2. Ina ladhaya UCHACHU ingawanitamusana. 3. Mara nyingiinarangiya KAHAWIA ILIYOKOLEA inayoendakwenye WEUSI

Read More »

KILIMO CHA BAMIA

 BAMIA Asili ya mboga hii ni Afrika ya Kati na ya Mashariki, lakini kwa sasa zao hili limekwisha enea katika sehemu nyingi za kitropiki, kama

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »