Sehemu ya Ghala la kuhifadhi vitunguu Saumu liliojengwa na MIVARF, lipo Mkoani Manyara Wilayani Mbulu, kijijini Bashay. Ghala hilo lina uwezo wa kuhifadhi tani 50 za vitunguu Saumu.
Na. Ibrahim Hamidu
Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) imeboresha Soko la Vitunguu Saumu kwa kujenga ghala la kuhifadhi vitunguu mkoani Manyara, wilayani Mbulu katika kijiji cha Bashay.
Ghala hilo lenye uwezo wa kuhifadhi tani 50 za vitunguu, limegharimu Jumla ya shilingi milioni 88 ikiwa MIVARF imechangia asilimia 95 ya fedha hizo na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imechangia asilimia 5 ya fedha hizo.
Akiongea na timu ya wataalam kutoka MIVARF ofisini kwake hivi karibuni wakati timu hiyo ilipokuwa ikikagua utekelezaji wa shughuli za Mradi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Nicholaus Haraba, alifafanua kuwa ujenzi wa ghala hilo umeongeza mnyororo wa thamani wa zao la vitunguu Wilayani Mbulu.

FAIDA ZA UTUMIAJI SAMADI MASHAMBANI
FAIDA ZA UTUMIAJI SAMADI MASHAMBANI : Samadi ni aina ya mbolea ambayo hutokana na vinyesi vya wanyama mbalimbali kama ng’ombe, kuku, mbuzi, kondoo na wengine. Hii