
MYCOTOXINS NI MOJA YA CHANGAMOTO KATIKA UZALISHAJI KUKU : Mycotoxins ni kemikali sumu zinazotolewa na fangasi (molds) na huathiri wanyama na binadamu. Sumu hizi pia hushika na kujiambukiza katika nafaka ambazo bado zipo shambani,wakati wa kuvuna, kusafirisha au kuhifadhi kwenye ghala katika hali ya unyevunyevu na wakati hali ya hewa inapobadilika.
Mycotoxins maarufu zinazoathiri ufugaji wa kuku ni kama ifuatavyo:
• Aflotoxins – hutolewa na Aspergillus flavus, Aspergillus parasiticas
• Ochratoxins – hutolewa na Aspergillus ochraceus
• Trichothecenes – hutolewa na Fusarium spp.
• Zearalenone – hutolewa na Fusarium spp
• Fumonisins – hutolewa na Fusarium spp.
Inakisiwa kuwa asilimia 25% ya mazao ya dunia huambukizwa mycotoxins na huleta hasara kubwa katika ufugaji wa kuku wa biashara.

Mycotoxins huathiri kuku kwa njia nne kubwa:
• Hupunguza hamu ya kula
• Hupunguza kufyonzwa kwa virutubisho vya chakula mwilini
• Huathiri mfumo mzima wa homoni za mwili
• Hupunguza kinga za mwili za kupambana na magonjwa. Na hili ndilo tatizo kubwa katika ufugaji kuku; kwa sababu huwafanya kuwa dhaifu katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali.
Pia mycotoxins hupunguza uwezo wa dawa za kutibu na kufanya kazi yake (Lower drug efficiency) na hupunguza uwezo wa chanjo kufanya kazi yake (Lower vaccine response)

Tatizo la mycotoxins pia ni changamoto kubwa kwa wazalishaji wa mazao ya mimea
KINGA
Ni vigumu kukinga maambukizo ya mazao kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, hata hivyo kutambua nafaka zilizoambukizwa ni jambo muhimu katika kupambana na sumu hizo.
• Kuangalia hali ya nafaka kwa macho na pia kupima katika maabara
• Kujitahidi kupunguza nafaka zisivunjike kwa wingi wakati wa kubangua
• Kuhifadhi nafaka vizuri, kuzuia unyevu, joto kali, wadudu waharibifu kama vile panya.
• Kwa nafaka zilizoanza kuathirika au kwa kukinga athari hizo njia pekee bora ni kutumia vifyonza sumu (mycotoxins adsorbent) kama vile MYCOBIND.
• Kuchanganya vitu ambavyo vinapambana na fangasi zinazotoa sumu kama aspergillus na fusarium kwa kuongeza kiasi cha tindikali katika vyakula na mifugo. Dawa za kuongeza tindikali katika vyakula ni kama vile FARMACID PREMIX.