Njia sahihi za kilimo bora

Share on facebook
Share on whatsapp
Share on twitter
Share on telegram
Soma kwa umakini itakuchukua dakika chini ya Kumi......
Udongo

Njia sahihi za kilimo chochote kile ambacho unatamani sana kukifanya zipo kanuni na taratibu zake za kuweza kufanya hivyo. Baadhi ya mambo ya msingi ambayo ni muhimu kuweza kufanya hivyo ni pamoja na;

Kutayarisha shamba mapema
Shamba ni lazima litayarishwe mapema. Matayarisho hayo ni pamoja na kufyeka, kukwatua na kulima.

Kutumia mbolea: 
SAMADI: Ihamishiwe shambani mapema kabla ya mvua kuanza.
MBOLEA ZA VIWANDANI: Tumia mbolea za kupandia kama vile Minjingu Rock Phosphate (MRP), DAP na NPK. Zikifuatiwa na za kukuzia kama UREA na CAN.

Upanda  mapema
Panda mara mvua za kwanza zinapoanza kunyesha.

Kutayarisha mbegu bora mapema
Nunua mbegu au tayarisha mbegu nzuri kutokana na mavuno yaliyopita kama ulitumia mbegu mchanganyiko.

Mbegu chotara (hybrid) zisirudiwe. Mbegu bora ziwe zilizopendekezwa kwenye ukanda/eneo lako.

Panda kwa nafasi zinazotakiwa
Hakikisha umepanda kila zao kwa nafasi maalum inayoshauriwa kitaalam. Rudishia mapema pale ambapo mbegu hazikuota.

Kupalilia vizuri na kwa wakati
Hakikisha shamba lako halina magugu wakati wote kwa kupalilia mapema. Wakati wa kupalilia punguzia miche na kuinulia matuta.

Kudhibiti magonjwa, wadudu na ndege waharibifu wa mazao
Tumia njia za kitaalam za kudhibiti magonjwa, wadudu na ndege waharibifu wa mazao.

Kuvuna mapema
Vuna mazao yako mapema mara yanapokomaa na kukauka vizuri. Vuna kwa wakati ili kuepuka mazao yako yasiharibike kwa jua, mvua na wadudu.

Kuhifadhi mazao vizuri
Mara baada ya kuvuna na kukausha mazao vyema, hifadhi kwenye vyombo vya kuhifadhia kama vile vihenge na magunia. Hakikisha umeweka dawa za kudhibiti wadudu waharibifu.

Kusafisha shamba mapema baada ya kuvuna.
Ng’oa mabua na masalia ya mazao na kuyalaza kati ya matuta na kuyafunika kwa udongo ili yaoze mapema. Kwa mazao ya tumbaku na pamba ng’oa na kuchoma moto mabua yake mapema.

PITIA
Umuhimu wa kitunguu swaumu katika kutibu magonjwa ya kuku
Diana Mussa

Diana Mussa

Mwana Blogger mahiri,aliyehama fani yake kutoka kwenye urembo na mitindo hadi kwenye uwanda wa kilimo ,na kuitumia sekta hii ya kilimo kwa kutoa taarifa zilizo sheheni mambo tele ~ na kushare kwa Watanzania,katika ulimwengu huu wa Teknolojia

Leave a Reply {Acha Maoni yako hapa}

Kuhusu Sisi

KilimoTanzania tumejikita kukupa Elimu pekee ya Kilimo kwa Gharama sawa na Bure, Ili tuweze kuwa na Taifa bora lenye wajisiriamali katika sekta ya kilimo na Ufugaji.

Kwa Mawasiliano usisite Kubonyeza hapa 

Vitabu Vya Kilimo na Ufugaji pia vinapatikana  Kwe Ukurasa Huu

Jiunge channel Yetu ya Telegram

Karibu uweze Kujiunga na Channel Yetu ya Telegram uwe wa Kwanza kupata ,Taarifa moya za kuhusu Kilimo mara zinapowekwa kwenye Tovuti Yetu

Nyaraka Mpya

Follow Us

Video Mbali mbali za Kilimo