Njoo ujifunze kilimo cha nyanya

NYANYA ni zao linalopendwa kutumiwa….kunogesha chakula, chakula kilichowekwa NYANYA huwa na radha nzuri inayomvutia mlaji
[​IMG]
Wakulima wengi hutamani kulima zao hili wengi huandika FAIDA na kusahau kujadili kuhusu HASARA zisababishwazo na kilimo cha zao hili.

[​IMG]
Kiukweli NYANYA inaweza ikakutoa ukafanikiwa ki maisha ila inaweza vile vile ikakupa hasara kubwa ukajuta kufanya kilimo cha zao hili.
[​IMG]
Andaa matuta vizuri lakini naomba nikwaMbie ndugu msomaji kila aina ya Tuta ina mahala pake na ardhi yake maalum hivyo ni bora kuichunguza ardhi yako vizuri maana kwa udongo wa kichanga ukiweka matuta ni dhahiri udongo utapelekwa na maji…kipindi cha kumwagilia.

[​IMG]
Zingatia nafasi katika upandaji wa zao hili la nyanya nafasi inayopendekezwa ni cm50 kutoka mche hadi mche mwingine …. usipande zao hili pasipo kufuata kanuni ya nafasi ya cm50 maana zao hili lina majani na ukipanda kwa kubananisha sana utasababisha joto kuzidi, vile vile matawi yakigusana kutoka mche mmoja kwenda mche mwingine unaweza kusababisha miche iambukizane magonjwa.
[​IMG]
Kwa kawaida zao hili huchukua siku 72 hadi 120 kupanda hadi kuanza kuvuna…
Zao la nyanya ni zao linalofyonza sana rutuba hivyo hakikisha ardhi unaiboresha kwa kuiweka mbole mara kwa mara…kwa mbolea za dukani Urea, dap, N.p.k, can na nyinginezo hakikisha unafuata maelekezo ya mtaalaam kabla ya kutumia hizo mbolea…mbolea ya Samadi au za mifugo hakikisha mbolea hizo ziwe zimekauka kabisa ziwe kama unga au kavu maana mbolea za mifugo zikiwa mbichi zitasababisha miche kuungua…na inaweza kudumaa pia.
[​IMG]
Nyanya inashambuliwa sana na wadudu ambao hupelekea zao hili kupata magonjwa hivyo kabla hujapanda zao hili hakikisha unaanda shamba na kupiga dawa za wadudu pamoja na dawa za magonjwa za ukungu. Ni vigumu sana kutibu nyanya pindi utakapoanza kuona dalili kwenye mche ulioathiriwa na magonjwa. Hivyo kipindi chote cha uhai wa nyanya ni lazima kuzingatia matumizi ya dawa.
[​IMG]
Endapo utagundua baadhi ya miche imepata maambukizi muone mtaalam wa madawa akushauri ukishindwa kuutibu ni bora ukaung’oa uo mche maana nayo huambukizana magonjwa kama tunavyoambukizana binaadam.
[​IMG]
Uhai wa nyanya unategemea Maji, Mbolea na Dawa japo baadhi ya wataalam hushauri kuongeza na busta…ila ndani ya baadhi ya hizi booster kuna kemikali inayozuru afya zetu…kama utaamua kutumia booster yoyote weka akilini kuwa ndani ya booster kuna kemikali…
Hivyo kwa ushauri wangu…ni bora mkulima ukatumia mbolea asilia, na maji….dawa usitumie mara kwa mara…
Tumia dawa wakati wa kuandaa shamba…
Tumia dawa kukinga magonjwa ya ukungu…
Tumia dawa kuangamiza wadudu waharibifu…
Tumia dawa kutibu miche iliyoathirika…
Ila dawa isitimike kwa kiwango kikubwa…na hakikisha unafata maelekezo ya dawa yaliyopo kwenye kibandiko.
[​IMG]
Kama utaihudumia miche ya nyanya vizuri kwa kuweka mbole pindi inapohitajika, kumwagia maji japo kwa wiki mara tatu…na hakikisha siku za kumwagia unamwagia asubuhi na jioni…Nyanya inaweza kuanza kutoa Vitumba (maua) ndani ya wiki ya 5 hadi ya 6 tuu tokea ulipoipanda.
[​IMG]
Unapopuliza madawa kuwa makini sana maana kipindi ambacho nyanya imeanza kutoa maua ni kipindi ambacho nyanya inahitaji uangalizi wa hali ya juu wanaita (INTENSIVE CARE)…kuna baadhi ya dawa ni marufuku kabisa kugusa maua hayo kwani hukausha kabisa hayo maua….
[​IMG]
Zao hili lina faida sana ukinunua mbegu kutoka kwa wauzaji makini unaweza kupata zaidi ya kilo 5 kwa kila mche japo zipo mbegu zinazo zaa hadi kilo 12 na kuendelea…na zipo pia mbegu ambazo ukianza kuvuna na ukiihidumia vizuri unaweza kuvuna zaidi ya miezi 6 hadi mwaka.
[​IMG]
Hasara kwenye kilimo cha nyanya mara nyingi husababishwa na uzembe….nasema ni uzembe kwasabu wengi tumejikuta tunakimbilia kilimo kwakuwa jirani amenunua pikipiki kwaajiri ya kilimo…na watu wengi husifia faida waliyopata pasipo kueleza na hasara walizopata….hivyo ukipiga dawa isiyosahihi upo uwezekano wa kuikosa miche yote….
Ukiweka mbolea vibaya upo uwezekano wa kuiunguza miche yote…
Usipo mwagia maji unaweza kuipoteza miche yote…
Usipo weka dawa kwa wakati unaweza kupoteza miche yote…hivyo ni jukumu letu wakulima kuzingatia uwekaji sahihi wa mbolea…kuzingatia uwekaji wa maji si lazima umwagie maji mengi eti ili kesho usimwagie mwagia majo kiasi cha kutosha ila usimwagie maji hadi matope yatapakae huku na huko…nyanya haihitaji maji kwa muda mrefu…itaoza….
Weka dawa kwa wakati…hapo utashinda na utapata faida ya uhakika….

PITIA
Fahamu Gharama Katika Kilimo cha Nyanya

 

source:https://www.jamiiforums.com/threads/njoo-ujifunze-kilimo-cha-nyanya.1263665/

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

Kilimo cha Maharage

Donec odio. Quisque volutpat mattis eros. Nullam malesuada erat ut turpis. Suspendisse urna nibh, viverra non, semper suscipit, posuere a, pede.

Read More »

Kahawa Inayoleta Utajiri

KAHAWA, ni zao kubwa la biashara, inachukua nafasi ya pili kwa  kuingizia taifa fedha nyingi za kigeni baada ya zao la Tumbaku, wakulima wengi wanaofuata

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »