Kilimo Bora cha maharage

UTANGULIZI
Maharage ni moja kati ya mazao ambayo yanalimwa sana na ni moja kati ya mazao yanayo waongezea kipato wakulima wengi sana nchini Tanzania lakn kwa kufuata kanuni za kilimo bora

MAHALI PA KUPANDA
Maharage hupandwa mahari kwenye muiniko wa mita 400-2000 kutopka usawa wa bahari kwenye udongo usio tuamisha maji

WAKATI WA KUPANDA
Sehem za umwagiliaji panda wakati wa kiangazi na sehem zenye mvua nyingi zinazo anza mwezi november hadi disemba april na may panda mwezi februali na machi.

MAANDALIZI

Shamba; lima shamba vizuri na kufukia yale magugu na lima kufuatana na mwinuko wa ardhi
mbegu; Andaa mbegu bora mapema kulingana na chaguo lako
mbolea;andaa mbolea kilo 75 DAP au 150 mijingu kilo 50 TSP na CAN kwa ekari

KUPANDA

Maharage yanatakiwa kupandwa eneo lenye unyevu wa kutosha weka ulefu wa sentimita 2.5 hadi 3 na fukia vizuri na hakikisha mbolea aigusani na mbegu kuepusha kuunguza mbegu.

na kwa maharage madogo ni kilo 25 had 30 kwa hekari na maharage makubwa ni kilo 40 48

kwa maharage pekee panda sm50 kati ya mstari na mstari na sm10 kati ya shina na shina

kwa kilimo mseto panda mahindi sm75 mstari na mstari na sm60 shina na shina weka mbegu 3 kwa maharage yanayo tambaa na 6 kwa maharage mafupi

PALIZI
Palizi inatakiwa kufanyika siku 14 baada ya maharage kuota na rudia tena kabla ya kuchanua. unaweza kutumia madawa ya kuuwa magugu kama galex,stomp, dual gold,sateca

WADUDU WAHARIBIFU
FUNZA WA MAHARAGE
ni wadudu wadogo wanao shambulia mimea michanga ya maharage wanaweza kusabisha uharibifu hadi kufikia asilimia 100
njia nzuri ya kuwazibiti ni kuwanynyuzia dawa mfano karate 5EC au actelic50 EC ndani ya sku nne hadi 5 baada ya maharage kuota

PITIA
KANUNI ZA MSINGI KATIKA KILIMO BORA CHA MABOGA

wadudu wengine ni wanao kula maua kutoboa vitumba na mbegu pamoja na wale wanao bungua ghalani

MAGONJWA
Magonjwa makubwa ni

ndui ya maharage
madoa pembe
kutu
magonjwa yanayo sababishwa na bakteria na virusi

punguza magonjwa hayo kwa kupanda mbegu safi, aina znazo vumilia na kutunza shamba na unaweza kutumia madawa kama
kocide,fugulani,Bayleton kwa kuzuia magonjwa yanayosababishwa na ukungu na bakteria

UVUNAJI
Maharage yanatakiwa kuvunwa pale yanapo kauka kuepusha kuoza na kupasuka na yanapo kauka piga vizuri mbegu zisipasuka au kuruka mbali
pepeta na chambua kuondoa uchafu anika yakauke vizuri kabla ya kuifadhi

HIFADHI
Ghara au chombo cha kuifadhia lazima kiwe safi na zuia wadudu kwa kutumia dawa asili na zaviwandani

NOTE; Maharage yanaweza kuzaa gunia 6 hadi 10 ukifuata kanuni bora za kilimo cha maharage

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

SABABU ZINAZOWEZA KUATHIRI CHANJO

SABABU ZINAZOWEZA KUATHIRI CHANJO SABABU ZINAZOWEZA KUATHIRI CHANJO KUTOA KINGA KWA KUKU INGAWA WAMECHANJWA : Uzoefu umeonyesha kuwa wafugaji wengi wa kuku wa kisasa(Commercial Chicken)

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »