MWONGOZO WA UZALISHAJI MAZAO KULINGANA NA KANDA ZA KILIMO ZA KIIKOLOJIA

Sh0.00

Category:

Sekta ya Kilimo ni mhimili wa uchumi wa Tanzania na imekuwa ikichangia Pato la mkulima
mmoja mmoja, kaya na Taifa kwa ujumla pia ni tegemeo la mapato ya fedha za ndani na za
nje ya nchi. Sekta hii imeajiri zaidi ya asilimia 70 ya idadi ya watu wote nchini na kuzalisha
mazao ya chakula na biashara. Mazao makuu ya chakula ya aina ya wanga yanayozalishwa
ni pamoja na mahindi, muhogo, mpunga na mtama. Mazao mengine ni ndizi, viazi vitamu na
viazi mviringo, ngano, ulezi na uwele. Mazao ya mikunde ni pamoja na maharage, kunde,
mbaazi, choroko na njegere. Mazao yote hayo ndiyo yanayochangia Taifa kujitosheleza kwa
chakula kwa zaidi ya asilimia 100. Mazao makuu ya biashara ni korosho, miwa kwa ajili ya
sukari, pamba, mkonge, tumbaku, pareto, kahawa na chai. Mazao mengine ni ya bustani na
mbegu za mafuta.

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “MWONGOZO WA UZALISHAJI MAZAO KULINGANA NA KANDA ZA KILIMO ZA KIIKOLOJIA”

Your email address will not be published. Required fields are marked *