TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI -kuidhinishwa matumizi ya aina mpya za mbegu za mazao

Share on facebook
Share on whatsapp
Share on twitter
Share on telegram
Soma kwa umakini itakuchukua dakika chini ya Kumi......

Kamati ya Taifa ya kupitisha Mbegu mpya (National Variety Release Committee-NVRC)
imepitisha matumizi ya aina 25 ya mbegu mpya za mazao mbalimbali ya kilimo. Mazao
hayo ni: Aina 3 za mahindi, 9 za maharage, 1 Mpunga, 3 Karanga, 2 Njugumawe, 2
Pamba, na aina 5 za Tumbaku. Hatua hiyo ya Kamati inalenga kuongeza uzalishaji na
tija, pamoja na kuinua kipato cha mkulima.
Pamoja na aina hizo 25 za Mbegu mpya za mazao mbalimbali zilizopitishwa, aina mbili
za Mbegu (Pamba na Mpunga) hazikupitishwa kwani hazikukidhi vigezo vya kisayansi.
Kupitishwa kwa aina hizo mpya za mbegu kunatokana na mapendekezo yaliyofanywa
na Kamati ya Taifa ya Kitaalamu ya Kuhakiki aina Mpya za Mbegu za Mazao (The
National Performance Trial Technical Committee), iliyofana vikao vyake tarehe 19-20
Oktoba, 2017 na 19 Januari, 2018 katika Kituo cha Utafiti wa Miwa Kibaha (SRI-Kibaha)
Aidha mbegu hizo mpya zimepitishwa baada ya kufanyiwa utafiti wa kina na
kugundulika kuwa zina sifa mbalimbali kama vile; kutoa mavuno mengi, ukinzani dhidi
ya magonjwa, kukomaa mapema na kupendwa na wakulima pamoja na walaji.
Mbegu hizi zimefanyiwa utafiti na vituo vya utafiti vya Umma na sekta binafsi hapa
nchini. Taasisi za utafiti za umma zimeongoza kwa kutoa jumla ya aina 17 za Mbegu

download PRESS_RELEASE.pdf

PITIA
Kilimo Bora cha maharage
Diana Mussa

Diana Mussa

Mwana Blogger mahiri,aliyehama fani yake kutoka kwenye urembo na mitindo hadi kwenye uwanda wa kilimo ,na kuitumia sekta hii ya kilimo kwa kutoa taarifa zilizo sheheni mambo tele ~ na kushare kwa Watanzania,katika ulimwengu huu wa Teknolojia

Leave a Reply {Acha Maoni yako hapa}

Kuhusu Sisi

KilimoTanzania tumejikita kukupa Elimu pekee ya Kilimo kwa Gharama sawa na Bure, Ili tuweze kuwa na Taifa bora lenye wajisiriamali katika sekta ya kilimo na Ufugaji.

Kwa Mawasiliano usisite Kubonyeza hapa 

Vitabu Vya Kilimo na Ufugaji pia vinapatikana  Kwe Ukurasa Huu

Jiunge channel Yetu ya Telegram

Karibu uweze Kujiunga na Channel Yetu ya Telegram uwe wa Kwanza kupata ,Taarifa moya za kuhusu Kilimo mara zinapowekwa kwenye Tovuti Yetu

Nyaraka Mpya

Follow Us

Video Mbali mbali za Kilimo