Kilimo cha Tangawizi

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin

Kilimo cha tangawizi kimekuwa kikiwapa unafuu wakulima wa sehemu nyingi hapa nchini hasa katika mkoa wa Kilimanjaro katika wilaya ya same
Tukisema kuna mikoa iliyo barikiwa Tanzania Kilimanjaro ni mojawapo hasa katika wilaya zake za Rombo Mwanga Hai na Same ambayo kama wilaya hizi zikipewa Ushirikiano wa moja kwa moja zinaweza kujitegemea zenyewe kwa kila kitu
Kwa kila wilaya katika mkoa ule a Kilimanjaro una umaarufu wake na wakipekee hasa katika Kilimo na biashara hata ya utalii
Ukiacha wilaya ya Mwanga inafatia wilaya ya Same ambayo kwa kweli katika makala hii nigependa kuzungumzia utajiri uliopo katika wilaya hii
Wilaya ya Same ambayo wasioijua wanaweza wakakuambia ni wilaya kame lakini huyo atakuwa anaijua kwa udogo wake
Lakini kwa sisis tunayoijua ukubwa wake ni wilaya tajiri yenye madini mengi, ardhi yenye rutuba na yenye kustawisha mazao ya aina tofauti na ye thamani kubwa na misitu mikubwa ile ya Shengena
Katika wilaya hii mbali ya mazao mengine inayolima kama mahindi, maharage, mpunga na miwa lakini kumeibuka zao la tangawizi ambalo ni utajiri mkubwa kwa wakulima wa Same
Asili ya zao hili ni maeneo ya kitropiki ya bara la Asia na hasa katika nchi za India na China na Jamaica ambazo ndizo zilizo gundua zao hili kama kiungo cha chakula.
hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Kigoma, Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na Kilimanjaro hasa katika wilaya ya Same.
Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1,500 au zaidi.
Huhitaji mvua kiasi cha mm.1,200-1,800 na joto la wastani wa nyuzi za sentigredi 20-25. Hustawi vyema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usiotuamisha maji.
Zao hili hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha na harufu katika vinywaji kama soda, juisi, vilevi na vyakula mbalimbali kama mikate, biskuti na keki.
Hata hivyo tangawizi hutumika pia katika kutengeneza madawa ya tiba mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi tumbo na pia hutumika katika vipodozi kama poda
Hivyo kutokana na matumizi mengi ya tangawizi pia yanaongeza umuhimu wake kwa jamii na soko kuwa kubwa ndani na nje ya nchi
Umuhimu wa zao hili katika Wilaya ya Same ulifanya viongozi wa vyama na serikali kuhakikisha kunakuwepo na kiwanda cha kushughulikia zao hilo
Mbugo wa jimbo hilo Mbunge Anne Kilango kwa ushirikiano na Naibu Waziri wa Kilimo, Dk David Mathayo kuanzishwa kiwanda hicho ambapo waliweza kumkaribisha Waziri mkuu panda katika uanzishaji na uendelezaji wake
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema kujengwa kwa kiwanda pekee cha kusindika tangawizi nchini kutakuwa ni mkombozi wa wakulima.
Kiwanda hicho kilichohamasishwa kwa kiasi kikubwa na Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anna Kilango Malecela kinajengwa eneo la Mamba Myamba Jimboni humo, moja kati ya maeneo yanayozalisha tangawizi kwa wingi.
Waziri Mkuu Pinda aliwaahidi wakulima na wananchi katika wilaya ya Same ambayo kuwa kiwanda hicho kinajengwa kwa ajili ya kumkomboa mkulima.
Alisema anatambua umuhimu mkubwa wa kiwanda hicho kwani kitaongeza thamani ya zao hilo hadi kufikia kati ya Sh4,000 na Sh15,000 kwa kilo moja ya tangawizi ya unga tofauti na ilivyo sasa ambapo mbichi ni Sh200 kwa kilo.
Mheshimiwa Pinda alisisistiza kuwa kiwanda hicho kitakamilika na kuanza uzalishaji kikiwa kimegharimu karibu Sh200 milioni.
Hata hiyo aliwaonya viongozi wa Ushirika wa Wakulima wa Tangawizi kutojihusisha na vitendo vya ubadhirifu vitakavyosababisha kufa kwa kiwanda hicho.
Pia aliliagiza Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo Nchini (Sido) kutoa utaalamu wa ujenzi wa kiwanda hicho.
Hata hivyo Naibu Waziri wa Kilimo, Dk David Mathayo, aliahidi kuendelea kupigania kupata miradi mingine ya maendeleo katika katika wilaya ya same mbali na kiwanda hicho.
Pamoja na hayo Dk David Mathayo Alisisitiza kuwa kilimo cha tangawizi kiwe endelevu na kuwataka wananchi kulinda vyanzo vya maji na kupiga marufuku uchimbaji wa madini katika msitu wa Shengena ambao ni chanzo cha mvua na maji
Niweza kuzungumza na wakuliama wa tangawizi kuhusu manufaa ya zao hili la tangawizi na ukilinganisha uanzishwaji wa kiwanda cha tangawizi
Mkulima asiyependa jina kutaja jina lake alisema kwamba mzao hili la tanagawizi limekuwa likiwaletea faida lakini wanapata shida katika utafutaji wa masoko hivyo kuanzishwa kwa kiwanda hicho kitawasaidia katika kupata soko la mazao yao
Mkulima mwingine alikuwa bwana Agree Justine ambaye ni mwenyekiti wa vijana wa kata ya Mamba Myamba na ambaye pia ni mgambo aliweza kuelezea aina za tangawizi na soko lake
Bwana Agree alisema kuna aina mbili za tangawizi wanazolima na zina soko kubwa na mavuno mengi.
Bwana agrey alisema kuwa kuna aina ijullikanayo kama Bombei ambayo asili yake ni kutoka India ambayo huzaa sana na huwa ndefu kati ya futi mbili hadi tatu na tunguu zake huwa ni nene
Aina ya pili bwana Agree alisema kuwa aina nyingine wao kama wakulima wanifaham ni ile ijulikanayo kama Poland inayotaka huko polland ambayo mbegu yake ni fupi inazaa sana na japo tunguu zake ni ndogo
Kuna uwezekana pia kiwanda kikiendeleza aina hizi kwa kutoa maelekezo yenye tija kwa wakulioma kutokana na aina hizi kuwa na soko kubwa alisema alisema agrey
Nilweza kukutana na mtaalamu mmoja wa mambo ya Kilimo na mifugo magreti Alocy Mbonea aliyeko moja ya vyuo marufu huko morogoro anasema tangawizi mbali na kuwa imebadilisha sana maisha ya watu lakini pia inauwezo kufanya Same chanzo muhimu cha mapato cha nchi
Magreti aloisi mkazi wa Gonja wilaya ya Same anaendelea kusema kuwa tangawizi imeweza kuwatoa wakulima wengi kutoka katika umaskini kwa kujiwekezea akiba na pia kujifunza Kilimo cha umwagiliaji
Hii inatokana na ukweli kwamba tangawizi inahitaji maji mengi hivyo kutengemea mvua kusingetosha hivyo kumfanya mkulima kujifunza Kilimo cha umwagiliaji
Hata hivyo magret alisema kuwa kiutaalamu mazao mengine huweza kupandwa katika shamba la tangawizi ili kuweka kivuli chepesi kitakachoweza kuhifadhi unyevu usipotee hivyo kumfanya mkulima kulima Kilimo mseto chenye manufaa mengi.
Pamoja na hayo bi magret alishauri vijana kkujituma zaidi na shughuli za Kilimo ktokana na kupewa kipaumbele sana badala ya kutokimbilia mjini kutafuta ajira zisizo halali
Nilipata fursa nikazungumza na vyanzo vya habari vya wizara ya Kilimo chakula na Ushirika kuhusu changamoto na magonjwa ambayo yameripotiwa kuhusiana zao hili la tangawizi
Zimekuwepo changamoto zinazopatikana katika zao hili ni magonjwa ya Madoa ya majani yanayosababishwa na viini vya magonjwa viitwavyo Colletotrichum zingiberis na Phyllosticta zingiberi ambao huathri zao la tangawizi.
Magonjwa haya huwasumbua sana wakulima na kuifanya tangawizi kutokuwa na ubora ule ulikuwa unategemewa na wakulima waliowengi wa same
Pamoja na hayo kuna matatizo ya Kuoza kwa tunguu ambapo husababishwa na viini viitwavyo Pithium na huathiri sana wakulima
Tangawizi inayolimwa Same huweza kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 9-10 baada ya kupanda, wakati majani yake yanapogeuka rangi kuwa njano na mashina kusinyaa.
Katika maeneo ya Mamba miamba huko mkoa wa Kilimanjaro mkulima wa tangawizi anaweza kuacha mazao yake shambani kwa misimu miwili na akavuna kwa kiasi kikubwa zaidi
Utaratibu huu wa kuacha zao kwa msimu mziama shambani ambao hufanywa katika zao la tangawizi humsaidia mkulima kuwinda soko la uhakika la bidhaa yake na kuliuza kwa msimu soko linapokuwa zuri
Hata hivyo Mavuno hutofautiana kulinganana na huduma ya zao, mavuno yanaweza kuwa kiasi cha tani 20-30 cha tangawizi mbichi huweza kupatikana.
Tangawizi iliyovunwa huweza kumenywa, kukatwa na kukaushwa juani au mara nyingine huchovywa katika maji yaliyochemka kwanza na ndipo kukaushwa au hukamuliwa mafuta.
Pia tangawizi husindikwa na kuhifadhiwa kwenye chupa zikiwa zimechanganywa na sukari au chumv ili kudumu kwa muda mrefui.
Mkulima wa tangawizi anajua ungumu wa kulima zao hili kutokana na kuhitaji maji mengi na mbolea pamoja na kupambana na magojwa hivyo hela nyingi inahitajika katika kuandaa zao hili ili liweze kuwa la kishindani
Serikali pia imetambua umuhimu wa zao hilo na kuamua kuhakikisha kuwa soko la tangawizi linapatikna na lenye uhakika
Pamoja na hayo serikali imeanzisha kiwanda cha tangawizi katika kata ya mamba miamba na kuwafanya wakulima wa tangawizi kupata sehemu ya kupumulia
Kiwanda hicho ambacho kinaweza kuanza mda wowote kuanzia mwezi wa tatu mwaka huu bna kuwafanya wakulima kukuongezeka na wngine kuongezea mashamba

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

Kilimo cha Tufaa

Tufaa ni tunda moja maarufu duniani ambalo hupendwa kuliwa na watu wa jamii zote, hii inatokana na utamu wake pamoja na faida za kiafya zinazopatikana

Read More »

Huu ni mfano wa Kuigwa

  Shamba la kilimo cha umwagiliaji cha Mbogamboga la Ngongoseke lililoko katika kijiji cha Nsola wilayani Magu ni mfano wa kuigwa katika matumizi ya ziwa

Read More »

SABABU ZINAZOWEZA KUATHIRI CHANJO

SABABU ZINAZOWEZA KUATHIRI CHANJO SABABU ZINAZOWEZA KUATHIRI CHANJO KUTOA KINGA KWA KUKU INGAWA WAMECHANJWA : Uzoefu umeonyesha kuwa wafugaji wengi wa kuku wa kisasa(Commercial Chicken)

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »