UFAHAMU UGONJWA WA MAFUA YA KUKU KIUNDANI ZAIDI.

Share on facebook
Share on twitter
Share on linkedin

 MAGONJWA YA KUKU/TIBA/KINGA.

Habari ya uzima ndugu mfugaji, ni matumaini yangu u mzima. Mimi ni mzima na leo tunaanza somo letu la magonjwa ya kuku, tutaongelea magonjwa ya kuku, dalili, tiba na chanjo endelea kuwa pamoja nasi.

FAIDA ZA KUZINGATIA TIBA/CHANJO.

•Hupunguza athari za kiuchumi zitokanazo na maambukizi. 
• Hulinda afya za kuku ambao hawajaambukizwa. 
• Hupunguza kuenea kwa maambukizi kutoka kuku wagonjwa kwenda kuku wasio wagonjwa. 
• Huwakinga wanadamu wasipate maambukizi kutoka kwa kuku wagonjwa. 
• Huzalisha kuku na bidhaa zenye ubora wa juu ambazo hupata bei nzuri sokoni.

Hatua Za Tahadhari Za Kuzuia Kuingia Na Kuenea kwa Magonjwa Shambani.

1. Tenganisha ndege kufuatana na aina ya ndege na umri wao 
2. Weka karantini kwa ndege/kuku wapya ili wachunguzwe kwa kipindi kisichopungua wiki mbili 
kabla ya kuingizwa shambani au bandani. 
3. Usiruhusu tabia ya kuchangia vifaa/vyombo kama vile makasha ya mayai, makreti ya kubebea kuku 
kati ya shamba na shamba, n.k. 
4. Wafanyakazi waanze kuwahudumia kuku wenye umri mdogo kabla ya wale wenye umri mkubwa. 
5. Usiruhusu watoto kucheza na kuku. 
6. Jaribu kuzuia idadi ya wageni wanaoingia shambani/bandani. 
7. Weka utaratibu wa kuangamiza mizoga ya kuku. 
8. Anzisha programu jumuishi ya kudhibiti wadudu/wanyama waharibifu. 
9. Panga utaratibu mzuri wa kuwapa kuku huduma ya maji na kufanya usafi. 
10. Panga utaratibu mzuri wa kuzoa taka na mizoga ya kuku. 
11. Panga utaratibu mzuri wa kusafisha banda na kupulizia dawa. 
12. Vifaa visafishwe na kuwekwa dawa ya kuua vijidudu kabla ya kuingizwa shambani. 
13. Hakikisha magari yanapoingia shambani yanapita katika kidimbwi chenye dawa ya kuua vimelea 
vya magonjwa. 
14. Hakikisha mfanyakazi anabadilisha viatu/mabuti kabla ya kuingia katika kila banda 
15. Weka taratibu nzuri za kuingia shambani, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha usafi wa viatu na mikono; 
au wageni na wafanyakazi kubadilisha nguo/viatu na kuvaa mabuti.

Ugonjwa ni nini?
Ugonjwa ni mabadiliko kutoka katika afya ya kawaida ya mnyama/kuku. Hali hii hutokea pale 
vimelea au vijidudu vinapoingia mwili wa mnyama, kwa kula vyakula vyenye sumu, au inapotokea kuna uhaba wa 
lishe au madini mwilini.

Tofauti za muonekano kati ya kuku mwenye afya na kuku mgonjwa

Kuku mwenye afya nzuri :
_Macho na sura angavu 
_Hupenda kula na kunywa maji 
_Pua zilizo safi, upanga na undu mwekundu, manyoya 
laini na yaliyopangika vizuri 
_Hupumua kwa utulivu 
_Sehemu ya kutolea haja huwa kavu 
_Kinyesi kikavu
_Hutaga mayai kawaida .

Kuku asiye na afya nzuri (mgonjwa)

_Huonekana mchovu na dhaifu 
_Hula na kunywa kidogo au zaidi ya kawaida 
_Hutoa kamasi puani, ute na matongotongo; manyoya 
yaliyovurugika 
_Hupumua kwa shida na kwa sauti 
_Sehemu ya kutolea haja inakuwa na unyevunyevu na 
kinyesi kuganda 
_Huharisha, mharo/kinyesi huwa na damu , kijani, cheupe, njano, kijivu au kuwa  minyoo Nk
_Hutaga mayai machache au husimama kutaga kabisa 
_Huwa na tabia ya kujitenga na wenzake katika kundi.

MAGONJWA YA KUKU.

Tuanze Na Mgonjwa Muhimu Yanayosababishwa Na Bakteria.

1. MAFUA YA KUKU

( infectious coryza) 
MAELEZO 
Ni ugonjwa unaoitwa infectious coryza huenezwa na 
bacteria. anaeitwa (hemophilus paragallinarum). 
Ugonjwa huu hushambulia kuku aina zote. Na usipo kuwa 
makini kwenye usafi wa banda na vyombo , kuruhusu watu kuingia ovyo bandani au kuku wa jirani kuja kuingia 
kwenye banda lako; ugonjwa huu unaweza shambulia kuku wako kwa kila wiki.

DALILI ZA UGONJWA HUU =
_Kuvimba uso chini na nyuma ya macho. 
_Kupumua kwa shida na kukoroma 
_Kutoka makamasi puani, 
_ Mdomoni kuwa na hali ya mterezo 
_Macho kuvimba
_Kushindwa kula. 
_Kupiga chafya , macho kuonekana kama yanatoka 
machozi

JINSI UGONJWA UNAVYOENEA: 
_Ugonjwa huu huenea kutokana kuku mmoja kwenda kwa 
kuku mwingine, au kutoka banda moja kwenda banda 
lingine. 
_Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilicho 
chafuliwa na kinyesi cha kuku Mgonjwa. 
_Ugonjwa huu uneea na kuambukizwa kwa mfumo wa 
hewa pale kuku wanapopiga chafya.

UNASHAURIWA 
Pindi ugonjwa unapo ingia bandani kwako wale kuku 
watakao onesha dalili za ugonjwa huu , watenge kisha 
wape tiba kuku wako wote; unatakiwa kuwatenga kwa ajili 
ya kupunguza maambukizi bandani.

DALILI ZA MZOGA UKIUPASUA
Usaha mweupe hadi njano huonekana kwenye macho na 
ndani ya pua

#MATIBABU 
Zipo dawa nyingi za kutibu ugonjwa huu antibiotic/ sulfa. 
Hizi ni baadhi tu. 
Fluban 
Flutan
Ganadexil 
Tylodox 
Teramycin.
Trimazine nk

:Tumia fluban,flutan kwa Kuku wanaooneshadalili za mafua bila vifo.

Tumia Ganadexil,tylodox kwa Kuku wenye mafua ambao 
kuna vifo vimetokea

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »