UFUGAJI WA BATA KAMA FURSA YA KIPATO

Share on facebook
Share on whatsapp
Share on twitter
Share on telegram
Soma kwa umakini itakuchukua dakika chini ya Kumi......

Ufugaji wa BataBata ni ndege kama walivyo kuku,kanga na wengine.

Bata ana urahisi mkubwa sana kumfuga kwakuwa hana complications katika matunzo yake mpaka kupata mazao yake.

Inashauriwa kumfuga bata katika eneo la kubwa kdg au katika banda maalum kwa wale wasio na eneo kuepuka uchafu unaweza kusambazwa na kinyesi chao.

Chakula cha bata ni Pumba za mahindi lakini pia bata anauwezo wa kula chakula cha aina yoyote ile kama mabaki ya ugali,wali,wadudu nk.

Bata mmoja maximum ana uwezo wa kutaga mpaka mayai 40 kwa zao moja na minimum mayai 15 mpaka 20 kwa zao moja.kwa hiyo bata ana uwezo wa kukuzaliana kwa wingi sana na kukuongezea kipato kwa muda mfupi.

Soko la bata ni kubwa sana ingawa hawaonekani masokoni kwakuwa wafugaji wa bata mijini si wengi kabisa lakini bata mmoja anakadiriwa kufikia shiling elfu 15 mpaka elfu 30.wateja wengi huwa wanafuata bata zizini baada ya kugundua walipo.so advertisement hapa inahusika kdg.

Moja katika uimara mkubwa wa bata huwa hawana magonjwa so ni nadra sana kwa bata kufa.na kama itatokea kufa basi ama bata amepigwa kichwani au kuungua nk.lkn kwa ujumla ukifuga bata mia unaweza wakuza wote mia bila shaka yoyote.so hawana risk kubwa kibiashara.

Bata hawahitaji madawa na chanjo kama walivyo kuku.kwa maana hiyo hutokuwa na gharama za madawa kama ilivyo kwa kuku.

Hebu tuone mchanganuo mdogo wa mradi huu.

Ukinunua bata majike 50 kwa kuanzia na madume 10.
50 × 15,000= 750,000/= Majike
10 × 20,000= 200,000/= madume.

Jumla itakugharimu kama sh. Milioni moja. Pamoja na usafiri.

Hapo chakula chao kwa bata 50 wanauwezo wa kula pumba debe 10 kwa mwezi na kila debe ni wastani wa sh. 3000 Elfu tatu. Chakula kwa mwezi kitakugharimu sh. 30,000/= Elfu thelathini hivi.

PITIA
Jifunze Kilimo Bora cha Karanga

Bata majike 50 kila mmoja akitaga mayai ya chini 20 ndani ya mwezi wa kwanza utakuwa na uhakika wa kupata bata
50 × 20 = 1,000. Bata elfu moja. Ambao utakuwa na uhakika kwamba lazima wakue wote kwa sababu ni wako free from magonjwa.

hivyo ukiwa na bata elfu moja ndani ya miezi 6 watakuwa tayari kuuzwa na kutaga upya .

Diana Mussa

Diana Mussa

Mwana Blogger mahiri,aliyehama fani yake kutoka kwenye urembo na mitindo hadi kwenye uwanda wa kilimo ,na kuitumia sekta hii ya kilimo kwa kutoa taarifa zilizo sheheni mambo tele ~ na kushare kwa Watanzania,katika ulimwengu huu wa Teknolojia

Leave a Reply {Acha Maoni yako hapa}

Kuhusu Sisi

KilimoTanzania tumejikita kukupa Elimu pekee ya Kilimo kwa Gharama sawa na Bure, Ili tuweze kuwa na Taifa bora lenye wajisiriamali katika sekta ya kilimo na Ufugaji.

Kwa Mawasiliano usisite Kubonyeza hapa 

Vitabu Vya Kilimo na Ufugaji pia vinapatikana  Kwe Ukurasa Huu

Jiunge channel Yetu ya Telegram

Karibu uweze Kujiunga na Channel Yetu ya Telegram uwe wa Kwanza kupata ,Taarifa moya za kuhusu Kilimo mara zinapowekwa kwenye Tovuti Yetu

Nyaraka Mpya

Follow Us

Video Mbali mbali za Kilimo