UFUGAJI WA BORA WA BATA MZINGA

UTANGULIZI
bata mzinga wanahitaji matunzo ya hali ya juu. Kwa kawaida bata mzinga hula chakula kingi kuliko kuku. Bei yake ni ghali zaidi. Kabla ya kuanza ufugaji wa bata mzinga ni lazima kuhakikisha una chakula cha kutosha kwa sababu ulishaji wa ndege hawa kadri wanavyokua huwa na gharama kubwa zaidi.

Ni muhimu pia kujifunza kwa undani na kufahamu namna ya kutunza vifaranga wa bata mzinga kwa kuwa hufa kwa urahisi sana. Pia, unapaswa kujikita kutafuta soko kwa sababu wanapokuwa ni vigumu kuwatunza kwa muda mrefu kutokana na ukubwa wa gharama ya chakula.

Wafugaji wachache kati ya wengi waliojaribu kuwafuga ndege hawa na kufanikiwa hata kufikia malengo yao ni kutokana na kuzingatia lishe kamili. Pamoja na hayo, wapo wafugaji ambao walishindwa kutokana na magonjwa pamoja na gharama ya utunzaji.

BANDA
Ni vyema banda liwe limesakafiwa au banda la asili la udongo usiotuhamisha maji. Pia, unaweza kutumia banda lenye mbao au mabanzi kwa chini. Unaweza pia kutandaza maranda kwenye mabanda. Hakikisha kuta za banda zimefunikwa vizuri ili kuwakinga dhidi ya baridi.

CHAKULA 
Chakula cha bata mzinga hakina tofauti na cha kuku. Vifaranga wanahitaji kupata lishe kamili yenye protini kwa wingi ili waweze kukua vizuri. Vifaranga kwa siku za awali wanahitaji kiasi cha asilimia 27 ya protini mpaka wanapofikia umri wa wiki sita.

Baada ya hapo mfugaji anaweza kupunguza hadi kufikia asilimia 18, na kuendelea hivyo hadi wanapokomaa.  Kutokana na gharama ya kununua chakula kuwa kubwa, unaweza kutumia reseheni ifuatayo kwa ajili ya kutengeneza chakula cha bata mzinga wewe mwenyewe.

MAHITAJI
Mahindi 5kg (yasiyokuwa na dawa)Karanga 5kgDagaa 5kgMashudu 10kgChokaa 5kg (chokaa inayotumika kwa lishe ya mifugo) . Namna ya kutengeneza chakula Twanga au saga pamoja kiasi cha kulainika kisha walishe vifaranga. Mchanganyiko huu hutegemeana na wingi wa bata mzinga unaowafuga. Hakikisha kila bata anapata chakula cha kutosha na chenye uwiano ulioelekezwa.

Pia waangalie mara kwa mara kuhakikisha wana chakula cha kutosha.
Uhifadhi: Hifadhi chakula cha ziada kwenye mifuko au debe kisha weka sehemu isiyo na unyevu.

KUTAGA
Bata mzinga huanza kutaga anapofikisha umri wa mwaka mmoja. Ndege hawa wana uwezo wa kutaga kati ya mayai 15 hadi 20 kwa mara ya kwanza na kisha kuhatamia. Anapoendelea kukua huweza kutaga hadi mayai 30. Hii ni kulingana na lishe nzuri atakayopatiwa.

KUHATAMIA
Bata mzinga anaweza kuhatamia mayai 17 hadi 20. Mayai hayo huhatamiwa kwa siku 28 na huanza kuanguliwa vifaranga kwa muda wa siku 3, kuanzia siku ya 28 hadi 31. Baada ya hapo mayai yaliyosalia bila kuanguliwa hutakiwa kutupwa kwa kuwa hayatoanguliwa tena na hayafai kwa matumizi mengine.

JINSI YA KULEA VIFARANGA WA BATA MZINGA
Vifaranga Wa bata mzinga ni tofauti na Wa kuku wakuku hutotolewa tayari wanajua kujifunza kula na kunywa Maji wakati Wa bata mzinga huzubaa kwa siku kama 4 ndipo wajue kula vizuri hivya wana hitaji uangalizi Wa hali ya juu sana. Hukaa kwenye brooder kwa muda Wa wiki 4 ambapo watahitaji joto la kutosha muda wote ambapo wiki ya kwanza watahitaji nyuzi joto 38 na na wiki ya pili utapunguza nyuzi joto 5 kila wiki utapunguza nyuzi joto 5.wanakuwa kwa haraka hivyo wanahitaji sehemu Kubwa ya kuwalea sentimita 20×20 kwa kila kifaranga kwenye wiki ya pili hadi ya Tatu.

Wanahitaji Chakula chenye protini nyingi 28% ktk Chakula chao kwa wiki 8 za mwanzoni hivyo ni bora kuwapa broiler starter kwa muda Wa miezi miwili. Maharisho ya sehemu ya kuwale (brooder) yanatakiwa yazingatie mambo yafuatayo:Kuwe kuna matandiko chini ya kutosha kiasi cha kina cha inch 3 ili kuweka hali ya joto.Matandiko yaweza kuwa maranda nyasi pumba za mpunga.Weka vyombo vya kulia Chakula na kunywea Maji kabla hujawaingiza Vifaranga hao.

PITIA
KILIMO BORA CHA ZABIBU - Jifunze Maarifa ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi

Weka vitu vya kung’aa ktk Chakula na Maji ili kuwa vutia kujifunza kula.Vitu vya kung’aa yaweza kuwa gololi zile za kuchezea watoto unatumbukiza kwenye Maji hivyo zile Rangi zitawavutia kusogea pale na kudonoa donoa au weka Maji ya Mchele km Maji yao ya kunywa ile Rangi nyeupe itawavutia kusogelea Maji hii ni namna ya kuwafunza kula au wachanganye na Vifaranga Wa kuku watajifunza kula kupitia Vifaranga Wa kuku.

Wape Chakula muda wate na wape Majani wiki ya pili maana 50% ya Chakula chao ni Majani Mboga Mboga mbichi. Wape joto kwa vyanzo vya joto ulivyo navyo kama taa za umeme 100w au 200w jiko la Mkaa taa ya chemli au kandiri au tumia Njia za asili.Kama ilivyo kwa kuku bata mzinga wanahitaji Dawa na chajo.

Wiki ya kwanza wape Newcastle vaccine wiki ya 4 wape fowl pox vaccine (ndui) wiki ya 6 wape Newcastle vaccine Utarudia baada ya miezi mitatu mitatu chanjo hii ya Newcastle.Wape vitamini na madini ktk Chakula chao.

Ikifika wiki ya 8 unaweza kuanza kuwatoa nje wajifunze mazingira ya nje na kujitafutia maana bata mzinga ni wajitafutiaji Chakula wazuri km kuku Wa kienyeji japo hupenda sana Majani.Ni vizuri kuwapa lusina mbichi hufanya vizuri ktk bata mzinga.Wiki ya 24 hadi 28 wanakuwa tayari wana kilo 8 hadi 12 hivyo wanaanza kutaga wachanganye na maduma katika ratio ya 1:5 yani dume 1 majike 5 hii ni kama bado hawajawa wazito sana kama wameshakuwa wazito au kuanze kuwa wavivu kuzeeka wawekee ratio ya 1:3 yani dume 1 majike 3.Bata mzinga hutaga kwa msimu kama walivyo kanga na hulalia siku 28 kama kanga na wanauwezo wakulalia Mayai yao 10 hadi 15 lakini hutaga mengi zaidi hivyo nivizuri ukatumia Mashine ya kutotolesha au kama una kuku Wa kienyeji anapo lalia unamuwekea ya bata mzinga Mayai 6.

Hivyo wakati huo bata anaendelea kutaga huku kuku wanalalia Mayai yao.Hivyo ni Njia nzuri maana bata mzinga wanatabia ya kususa Mayai yao km MTU ukiyashika na marashi au yakipata harufu ambayo sio yake.

MAJI
Kama ilivyo ndege wengine, bata mzinga pia wanahitaji kupatiwa maji masafi na ya kutosha wakati wote. Wawekee maji katika chombo ambacho hawatamwaga na wanakifikia vizuri. Hakikisha maji hayamwagiki bandani kwani kwa kufanya hivyo banda litachafuka na kukaribisha magonjwa kwa urahisi. Ni vizuri kuwalisha bata mzinga vyakula vingine kama majani. Majani husaidia kuwapatia protini: mfano; kunde, fiwi na aina nyingine za majani jamii ya mikunde huhitajika zaidi kwa kiasi cha 25% hadi 30%.

MAGONJWA
Bata mzinga hushambuliwa na magonjwa kama taifodi, mafua na kuharisha damu. Wanapougua ni rahisi kuambukiza kuku, bata na ndege wengine wanaofugwa kwa haraka sana. Pia, ndege hawa husumbuliwa na viroboto wanaosababishwa na uchafu wa banda hasa linapokuwa na vumbi.

CHANJO
Bata mzinga wanatakiwa kupatiwa chanjo ya ndui (mara moja kila mwaka), kideri (kila baada ya miezi mitatu), gumboro (kwa muda wa wiki tano – ukiwapa jumatatu, basi unawapatia kila jumatatu ya wiki), na vitamini A mara baada ya kuanguliwa.

MAGONJWA MAKUU YA NDEGE
Magonjwa huainishwa kulingana na baiolojia yao,kama Virusi, Bakteria,Kupe,ukungu,na chanzo chao,kwa mfano magonjwa ya lishe yaliyoangaliwa hapo juu.Hata hivyo,magonjwa makuu katika ndege yamegawanywa katika makundi matatu kulingana na makali yao na umuhimu katika mfumo wa uzalishhaji mdogo katika vijiji.Vitu muhimu kama tabia zao wakati wa mlipuko(dalili),na matibabu yanayowezekana(kuzuia ama kudhibiti)vile vile wakati wa kutokea magonjwa hayo.Umuhimu wa ugonjwa huthaminiwa na idadi ya vifo na athari kwa uzalishaji,na itatofautiana kutoka eneo hadi eneo na msimu hadi msimu.

PITIA
MATUMIZI YA UHAKIKA YA DAWA ZA KUDHIBITI VIUMBE HAI TEGEMEZI WA MIFUGO

MCHANGANYIKO WA MAGONJWA
Magonjwa kadhaa yasiyo maku yanaweza kukutana na magonjwa mengine na kusababisha madhara makali kwa ndege.Hii ndio hali kwa mfano maambukizo ya E.coli, utapiamlo na kupe wa ndani. Magonjwa kama haya ni vigumu kuua ndege lakini huwa na madhara makubwa kwa kinga ya ndege dhidi ya magonjwa,na kujenga msingi wa maambukizo rahisi ya magonjwa mengine baada ya kuwafanya ndege kuwa dhaifu kiafya. Umuhimu mkubwa huashiria ugonjwa wa kawaida wenye vifo vingi(zaidi ya asilimia 30 ya kundi),husambaa kwa urahisi na ni vigumu kutibu au hautibiki kabisa.Umuhimu wa wastaani kawaida ,vifo vya wastani(10-30%) kwa kundi na /ama vigumu kutibu.Ugonjwa usio mkuu huashiria wa kawaida, vifo vichache na /ama rahisi kutibu.

UGONJWA WA KUAMBUKIZANA WA KUKU UNAOSHAMBULIA MAPAFU NA MFUMO WA NEVA – NEWCASTLE DISEASE (NCD)
Ugonjwa huu huua, ni wa kawaida katika msimu wa mvua,na hutokea mara kwa mara katika vifaranga wachanga,lakini pia katika kuku waliokomaa.Vifo vya juu katika kundi,mara kwa mara baina ya aslimia 30 na asilimia 80 ya ndege hufa,ugonjwa unapowakumbaKuku hupoteza hamu ya kula na usagaji mbaya wa chakula tumboni. Unaweza kuonyesha upumuaji mzito,kinyesi cha kijani na wakati mwingine kuhara damu.

Unaweza kuonyesha dalili za kuchanganyikiwa,kiharusi na hufa ghafla.Dalili zinaweza kutokea zote wakati mmoja.Ugonjwa huu ni wa virusi (virus)kwa hivyo hauna tiba,lakini unaweza kuzuiwa kwa kuwachanja ndege wote ukijumuisha vifaranga wa kutoka wiki mbili.

HOMA YA NDEGE – AVIAN INFLUENZA(AI)
Ugonjwa huu hubebwa na bata na bata maji,na unaweza kusambaa kwa urahisi na ni hatari sana kwa kuku.Vifo vya juu katika kundi,ndevu na panga za jogoo huvimba na kuwa na rangi ya kibuluu (samawati).

Husambaa kupitia chakula na maji yaliyochafuliwa katika madimbwi na vyombo vya maji/chakula.Ugonjwa huu husababishwa na virusi (virus),kwa hivyo hauna tiba. Ili kujikinga na ugonjwa huu zingatia usafi kwenye banda lako na vyombo vya kuku, ukiona dalili za ugonjwa huu waondoe kuku wagonjwa, wachinjwe na kuchomwa moto. Kabla ya kuingiza kundi lingine la kuku kwenye banda lenye ugonjwa hakikisha unapulizia dawa za kuua virusi ka a VIRU KILL.  Mara uonapo dalili za ugonjwa huu muite afisa ugani wa mifugo (Veterinarian)

NDUI YA KUKU – FOWL POX
Huonekana mara kwa mara katika vifaranga wadogo,lakini pia kwenye kuku waliokomaa na huonekana uvimbe mdogo mdogo kwenye ndevu,panga na uso wa kuku.joto la kuku hupanda,uchovu unaoambatana na vifo vya ghafla.Ugonjwa huu ni wa kawaida wakati wa msimu wa kiangazi,lakini pia unaweza kutokea mwaka mzima.Ugonjwa huu ni virusi kwa hivyo hauna tiba.Chanjo inapatikana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo.

UGONJWA WA MAREK – MAREK DISEASE
Huonekana tu katika ndege walio na zaidi ya wiki 16 kwa hiyo hauwapati kuku wa nyama labda kama umewafuga kwa ajili ya uzalishaji (parent stock).Mwanzoni ndege wanaweza kuonyesha bawa moja kushuka au yote mawili.Ama mguu mmoja ama yote inaweza kupooza.Ugonjwa huu ni virusi,kwa hivyo hauna tiba,lakini Chanjo inapatikana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo.

MAAMBUKIZO YA BAKTERIA WA E.coli
Hutokea sana sana katika vifaranga walioanguliwa (Day old chicks),na husababisha maambukizo katika tumbo.Dalili katika ndege wakubwa:kupumua kwa tabu au maambukizo katika mayai na kupungua au kuacha kabisa kwa utagaji kwa kuku wa mayai, kinga bora ni usafi katika mayai kwa ajili ya .Tiba kwa vifaranga wagonjwa inawezekana ukiwa na kiua vijisumu (antibiotics) kama OTC 10%, 20%, 30%.

KIPINDUPINDU CHA KUKU – pasteurellosis
Unaweza kutokea wakati wowote na kwa rika zote.Dalili ni kuharisha sana kwa kuku,kupumua kwa tabu,kukosa hamu ya kula,ndevu na panga za jogoo huwa na rangi ya kibuluu(samawati).Unaweza kutokea kama ugonjwa sugu na kuku kufariki ghafla .Mambukizo kupitia chakula na maji yaliyochafuliwa.Hauna tiba.kinga ni usafi wa hali ya juu na chanjo.Ua na uchome moto kuku wote walioathirika.Chanjo inapatikana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo.

PITIA
DUME ZURI KWA UZALISHAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA

UGONJWA WA KUHARA VIFARANGA
Ugonjwa huu unasababishwa na bacteria aina ya salmonella pullorum(Bacillary white bacteria)
Hutokea sana sana katika vifaranga wadogo.Vifaranga hutembea kwa tabu sana,tumbo huvimba na hukokota mbawa zao.Kinyesi chao huwa maji maji na hugeuka cheupe.Hauna tiba.Kuzuia ni kutilia usafi maanani.Ikiwa ugonjwa utatokea,tenga ama ua na uchome ndege.Ugonjwa huu husambazwa kwa kifaranga kutoka kwa mayai ya kuku aliyeathirika,ambaye haonyeshi daalili zozote za kuwa mgonjwa.

HOMA YA MATUMBO YA KUKU – TYPHOID
Huonekana zaidi kwenye kuku wakubwa.Dalili:joto huwa kali,uchovu,panga na ndevu za kuku huwa za kibuluu (samawati).Hauna tiba.Kinga ni kutilia usafi maanani na kuua kuku wagonjwa.Usinunue vifaranga kutoka kwenye vyanzo ambavyo hauvijui,na usitumie mayai kwa ajili ya kuanguliwa kutoka kwenye kuku wagonjwa.

GUMBORO – Infectious Bursal Disease(IBD)
Huonekana tu katika vifaranga walio chini ya wiki 6,na ni wa kawaida katika makundi makubwa ambayo yamefugwa katika sehemu zilizofungwa (indoor).Sio wa kawaida katika mfumo mdogo wa ufugaji vijijini.Dalili za kawaida: kuharisha.Ugonjwa huu ni virusi ,kwa hivyo hauna tiba.Chanjo inapatikana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo.

UGONJWA WA KUPUMUA 
Dalili:Pua inayotoka makamasi,uvimbe chini ya macho,macho yaliyojifunga,upungufu katika utagaji wa mayai.Tiba ni kuongeza kiua vijisumu (antibotics) katika maji ya kunywa.

UGONJWA SUGU WA KUPUMUA – Mycoplsmosis
Dalili:Pua inayotoka makamasi ama iliyoziba,uso uliovimba,macho yaliyojifunga,upungufu katika utagaji wa mayai,vifo visivyo vya kawaida.Tiba ni kuongeza kiua vijasumu (antibotics)katika maji ya kunywa.

COCCIDIOSIS 
Ugonjwa huu unaweza kutokea wakati wowote na katika rika zote,lakini unaweza kuzuiwa kwa kusafisha kwa makini nyumba za ndege.Dalili:hali dhoofu ya kuku,kuchoka,kutembea kichwa chini ,manyoya yaliyotimka,kuhara damu.Vifo katika vifaranga wachanga.Ikiwa vifaranga wataendelea kuishi watabakia kuwa wembamba na watachelewa kutaga.Tiba:Weka dawa ya Coccidiostatics katika maji ya kunywa au chakula.Kuzuia:Usiweke ndege wengi pamoja.Epuka kuweka ndege wa rika mbalimbali katika nyumba moja kwani ugonjwa unaweza kusambaa kutoka kwenye kuku wakubwa hadi kwa vifaranga.

MINYOO
Minyoo ni vimelea vya ndani na ni vya kawaida katika umri wote katika mfumo wa uzalishaji vijijini na mjini.Vimelea hivi husababisha afya mbovu,kupoteza uzito,kupungua kwa uzalishaji wa mayai.Tiba bora ni kuongeza dawa ya minyoo kama piperazine katika maji ya kunywa mara moja ama mbili kwa mwaka,ikiwezekana wiki mbili kabla ya chanjo yoyote.

CHAWA, KUPE, VIROBOTO NA UTITIRI
Huvamia rika zote wakati wowote,lakini hutokea mara kwa mara katika nyumba za kuku zenye unyevunyevu na uchafu. Ndege waliokomaa husumbuliwa na hutumia wakati mwingi wakidonoa na kujikuna.Vifaranga wachanga wanaweza kufa kwa sababu ya upungufu wa damu (anaemia).

Kama hautatibiwa utitiri,chawa,viroboto,kupe watasababisha kuku kupungua uzito na pia kuna uwezekano wa kupoteza manyoya kwa sababu ya kunyonywa damu na vimelea na kuwashwa na ngozi.Chawa wanaweza kuonekana karibu na macho na pua.Viroboto vinaweza kuonekana kwenye tumbo.Tiba:Nyunyiza dawa ya kuua vimelea kama Akheri powder,jivu na mafuta. Jivu na poda ya salfa inaweza kutumiwa mahali ambapo kuku huoga na mchanga.Viota vinaweza kulindwa kwa kuwekewa majani kadhaa ya tumbaku yaliyochanganywa na jivu katika viota.

MAGAMBA KWENYE MIGUU
Miguu yenye magamba husababishwa na vimelea vya nje vinavyowasha ngozi kwenye miguu ya ndege.Dalili:Miguu ina magamba yanayoonekana na majeraha na anaweza kulemazwa katika kutembea.Tiba:Weka miguu kila siku kwenye mafuta taa,ama katika dawa kuogeshea mifugo hadi magamba yatoweke.

LISHE DUNI Ndege wanaoathirika zaidi ni wale wanaofugwa ndani kuliko wale wanaojtafutia chakulaDalili:mifupa kukua vibaya na kunyonyoka manyoya.Ndege hutembea kwa tabu;huchopea .Tiba,ukigundua mapema wape ndege wako vitamini na kalsiam ya ziada kwenye chakula, pia wape majani, mabaki ya mboga za majani

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

KILIMO BORA CHA VIAZI MVIRINGO

                                               UTANGULIZI Viazi mviringo ni zao muhimu la chakula na biashara katika nchi nyingi zinazoendelea. viazi husitawi vizuri sehemu zenye miinuko kati ya mita

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »