UFUGAJI WA KAMBARE KITAALAMU I

UFUGAJI WA KAMBARE KITAALAMU

FAIDA ZA KUFUGA KAMBARE

• Kambare ni aina ya samaki wanaoweza kukua hadi kufi kia kilo 10 na hivyo humuwezesha mfugaji kujipatia kipato na nyama zaidi kuliko perege na aina nyingine za samaki.

• Nyama ya kambare imethibitishwa kuwa na kirutubisho kijulikanacho kama Omega-3, ambacho humpunguzia mlaji uwezekano wa kupata athari za magonjwa mbalimbali kama vile saratani, shinikizo la damu, na magonjwa ya akili.

− Kambare wanapofugwa pamoja na perege (kambare mmoja kwa kila perege wanne mpaka watano), hudhibiti mazaliano ya perege, hivyo kuwawezesha kukua hadi kufikia uzito mkubwa (mpaka kilo 5).

− Vilevile kambare hupunguza kuzaliana ovyo kwa vyura kwenye mabwawa kwa kula mayai na vifaranga vyao. Vyura ni hatari kwani hula aina nyingine za samaki kama perege.

− Nyama ya kambare waliofugwa kwenye matengi au mabwawa ni salama kiafya kuliko wale wanaovuliwa kwenye mito kwani nyama yao ina uwezekano mkubwa wa kuwa na takataka za sumu.

AINA ZA KAMBARE ZINAZOPENDEKEZWA KWA WAFUGAJI WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI:

• Kuna aina nyingi za kambare zipatikanazo Afrika lakini wengi wao hawafai kufugwa kwa sababu ni wadogo na hawastawi vyema ndani ya matangi au mabwawa.

• Aina maarufu inayopendekezwa kufugwa katika ukanda wa Afrika Mashariki ni ile ijulikanayo kitaalamu kama African catfish.

MFANO WA SEHEMU ZA KUTENGENEZEA BWAWA LA SAMAKI
MFANO WA SEHEMU ZA KUTENGENEZEA BWAWA LA SAMAKI

NAMNA AMBAVYO MFUGAJI ATAVYOWEZA KUFUGA KAMBARE:

1. Chunguza kama kuna soko zuri la kambare la kuweza kukupatia faida:

• Inapasa kuwa na uamuzi sahihi iwapo unahitaji kufuga kambare ili kujipatia kitoweo, kuuza au kuuza vifaranga vyake (kwa kawaida vifaranga huwa ni wadogo mithili ya vidole vya binaadamu) na mara nyingi hutumika kama chambo cha kuvulia samaki wakubwa au vifaranga kwa ajili ya kufugwa ili wakue.

PITIA
UFUGAJI BORA WA SUNGURA KIBIASHARA

• Tayarisha mchanganuo mzima wa gharama za ufugaji (kwa mfano gharama za ujenzi wa bwawa, chakula nakadhalika) na mapato unayotarajia kuyapata na utathmini kama utapata faida.

2. Hakikisha unavyo vyanzo vya uhakika vya kujipatia vifaranga (mara nyingi kutoka kwa mabwana samaki), chakula na maji. Vilevile unaweza kujipatia vifaranga kutoka mabwawa mengine jirani.

• Inapasa kufahamu kwamba ni mara chache kambare huweza kutaga mayai yao kwenye matangi au mabwawa yaliyochimbwa. Hivyo uzalishaji wa vifaranga hivi hufanywa kwa kuhamasisha kambare majike kwa kuwadunga sindano zenye vichocheo maalum (hormones) au kwa kuwakamua majike ili kupata mayai na kuyachanganya na mbegu za madume na kuhifadhiwa kwenye chombo maalum (incubator) ndipo vifaranga hupatikana.

• Kwa vile uzalishaji na utunzaji wa vifaranga huhitaji vifaa maalum maarifa na uzoefu wa kutosha, mfugaji anaweza kupata haya kutoka kwenye miradi ya namna hiyo iliyopata mafanikio katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, pia ni rahisi kwa wafugaji kuweza kujipatia vifaranga kutoka kwenye vyanzo hivyo.

3. Chagua eneo linalofaa kwa ujenzi wa bwawa au matangi na toa kipaumbele kwenye mambo yafutayo:

• Aina ya udongo: Udongo wa mfinyazi ndiyo unaofaa, iwapo ardhi ya mahala hapo ni ya kichanga basi ni vyema ukadhatiti kingo na sakafu za bwawa lako ili kudhibiti mmomonyoko wa udongo na upotevu wa maji.

• Mitiririko ya maji: Chagua eneo lenye mteremko au mwinamo ili iwe rahisi kwako kukausha bwawa wakati inapohitajika kufanya hivyo, iwapo itakuwa vigumu kupata mteremko basi huna budi kuwa unayatoa maji kwa kuyamwaga nje ya bwawa. Pia chagua sehemu ambayo haitoweza kuathiriwa na mafuriko ya mito au maji yanayotirikia bwawani.

PITIA
KANUNI ZA MSINGI ZA UFUGAJI BORA WA SUNGURA

4. USANIFU NA UJENZI WA BWAWA :

Ukubwa na umbo la bwawa: Bwawa lenye vipimo chini ya mita za mraba 400 huchukuliwa kama ni dogo na lile lenye vipimo zaidi ya mita za mraba 400 ndilo linalofaa. Bwawa lazima liwe na umbo la mraba au mstatili. Na kadiri bwawa linavyokuwa kubwa ndivyo uwezekano wa kufuga kambare unavyokuwa mkubwa, Hii ni kwa sababu:

• Bwawa linapokuwa kubwa linaongeza uwezekano mkubwa wa samaki wako kuweza kujipatia kirahisi virutubisho asilia na hewa safi kuliko linapokuwa dogo.

• Inakuwa vigumu kwa wadudu waharibifu kuwaona kirahisi samaki wako.

• Ni vigumu kwa magonjwa na magugu kusambaa haraka.

• Si rahisi kwa takataka na udongo unaoletwa na mafuriko au mvua kujaza kwenye bwawa.

KINA NA MWINAMO WA BWAWA:

Kwa bwawa la wastani kina cha chini kinachopendekezwa kiwe nusu mita na kina kirefu kiwa mita 0.8 na kwa bwawa kubwa kina kiwe mita 0.6 hadi mita 1.2. vina hivi huwezesha kupatikana mwinamo sahihi unaohitajika kwenye sakafu ya bwawa.

WATAALAM WAKIKAGUA BWAWA LA KAMBARE
WATAALAM WAKIKAGUA BWAWA LA KAMBARE

JINSI YA KUTIRIRISHA MAJI KWENYE MATANGI AU BWAWA LA KUFUGIA:

• Wakulima wengine hutilia mkazo mfumo wa kujenga mabwawa madogo (yaani vifaranga 4 hadi 6 kwa mita moja ya mraba) unaoruhusu kutiririsha na kuyaondosha maji wakati wote toka bwawani.

• Hata hivyo mfumo huu hautoi nafasi kwa bwawa kurutubishwa kwa ajili ya ustawi wa vijimea ndani ya maji (phytoplankton) au miwani (algae) kwa vile maji yanayotiririshwa huondosha rutuba zote ndani ya bwawa. Hivyo inapasa mfugaji kulirutubisha bwawa lake mara kwa mara.

• Vilevile pale ambapo mfumo huu utatumika basi pawepo na kizuizi cha maji kuingia bwawani wakati mfugaji anarutubisha bwawa na matoleo ya maji toka bwawani au kwenye matangi wakati yanapohitajika hususani wakati wa uvunaji.

PITIA
MATUMIZI YA UHAKIKA YA DAWA ZA KUDHIBITI VIUMBE HAI TEGEMEZI WA MIFUGO

• Pia pawepo na matoleo ya maji ya ziada ili kuepuka mafuriko ya maji bwawani wakati wa mvua kubwa, hali ambayo inaweza kusababisha upotevu wa samaki. Tengeneza toleo la maji toka bwawani kuelekea upande wa juu mwisho wa kingo za bwawa kiasi cha sentimita 6 kutoka juu na weka wavu mwembamba ili kuzuia samaki wasisombwe na maji yanayotoka bwawani.

• Iwapo mfumo huu unatumika, maji lazima yaingizwe na kutolewa bwawani au kwenye matangi wakati wote ili kuhakikisha samaki wanapata kiasi cha kutosha cha hewa safi . Vilevile samaki wapatiwe chakula chenye virutubisho vyote vinavyohitajika ili waweze kukua
vizuri.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

KILIMO CHA UYOGA

Kwa kuwa #uyoga upo wa aina mbalimbali, usitawishaji wake hutofautiana katika mahitaji yake, ikiwa ni pamoja na hali ya hewa, malighafi za #kuoteshea, urahisi wa

Read More »

Kilimo cha Mpunga Tanzania

MPUNGAHili ni zao la chakula linalolimwa kwa wingi kwenye maeneo ya ukanda wa joto. Zao hili linastawi zaidi kwenye udongo wa tifu tifu na eneo

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »