UFUGAJI WA KUKU WA MAYAI HATUA KWA HATUA

Ufugaji wa kuku wa mayai katika Makala hii ya ufugaji wa hatua kwa hatua nitaelezea ufugaji wa kuku wa mayai kwa lengo la uzalishaji wa mayai kibiashara. Nimelenga ufugaji utakaomtoa mfugaji kutoa hatua moja kwenda nyingine na si ufugaji wa mazoea. Kuku wa mayai ni kuku maalumu kwa ajili ya utagaji wa mayai na uleaji wake unapaswa uangaliwe kwa umakini tangu kifaranga kikiwa na siku moja na kuendelea hadi kuku anapofikia umri wa kuanza kutaga mayai na kuendelea. Ufugaji wa kuku wa mayai umegawanyika katika hatua tano kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini. Hatua hizi zimepangwa kwa kuangalia (1) ukuaji (2) Mahitaji ya nafasi kwenye nyumba na (3) Aina ya chakula anachotakiwa kupewa.

[ninja_tables id=”1105″]

Kwa kawaida kuku wa mayai huanza kutaga mayai wakifikisha wiki 18 hadi 20 na wataendelea kutaga mfululizo hadi watakapofikisha wiki ya 72 hadi 78. Wachache watafika wiki 120 kama inavyoonyeshwa kwenye jwadwali hapo juu. Katika mfuatano wa Makala hizi nitaelezea hatua zote za ukuaji wa kuku wa mayai na nini cha kufanya kwa kila hatua ili uweze kupata uzalishaji unaotegemewa kwa kuku wako.

Endelea kufuatilia makala hizi za ufugaji wa kuku wa mayai hatua kwa hatua na katika hatua ya kwanza itakayokujia hivi karibuni itahusu Maandalizi ya awali ya ufugaji wa kuku wa mayai. Itakuelewesha nini cha kufanya katika hatua za mwanzo za mradi wako wa ufugaji wa kuku wa mayai. Karibu Fuga Kibiashara.

ufugaji wa kuku wa mayai

PITIA
DUME ZURI KWA UZALISHAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

ZIJUE FAIDA ZA KULIMA MAPAPAI

Hili ni aina ya zao la matunda linalopatikana katika familia ya caricaceae na linajulikana kwa jina la kisayansi carica papayaPapai ni moja ya matunda ambayo huchukua

Read More »

Kilimo cha Kunde

KUNDE – COWPEAS (vigna unguiculata) UTANGULIZI Kunde ni zao ambalo linaweza kulimwa kwa ajili ya chakula na bishara ni zoa lenye kiasi kukubwa cha protini

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »