UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA [ BROILER ]

UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA
Katika ufugaji inawenzekana umekuwa ukiona Miradi ya watu jinsi ilivyo mikubwa. Unapenda sana kutembelea katika miradi mbalimbali, pia na wewe unawazo la kufuga lakini unashindwa kujua ni mtaji sh ngapi utakao tosha kuanzia mradi wa ufugaji kuku.
Ndugu sio lazima wewe kuanzisha mradi Mkubwa kama unayo iona ya wengine. Hao mpaka kufikia hapo wamechukua muda kidogo na wamekutana na changamoto nyingi.
 Hivyo hata kwa mtaji mdogo kabisa unaweza azisha mradi wako wa ufugaji kuku na baada ya muda nawewe utakuja kutembelewa katika mradi wako.
Katika ufugaji kuku kuna aina nyingi za kuku Leo tuangalie ufugaji wa kuku wa nyama broiler.
Kila aina ya kuku kuna vitu za muhimu haya ni mahitaji ya ufugaji kuku wa nyama broiler
@Eneo
@Mtaji
@Banda
@Vifaa
@Chakula/maji
@Madawa
@Vifaranga
Hayo ndio mahitaji kwa kuku broiler hapa Leo hatuta ongelea hayo mahitaji, tutaongelea  gharama za matunzo kuanzia kununua vifaranga hadi kuuza na faida yake ipoje! Kwa kawaida watu hujua kufuga kuku ni mpaka uwe na mtaji Mkubwa hapana! Hata mtaji wa Laki 5 unaweza fuga kuku broiler  na ukapata faida zuri na jinsi utakavyo endelea kufuga mtaji wako utaendelea kukuwa.
Hapa tunaanza kwa mtaji mdogo wa kuanza na vifaranga 100
Kuna makapuni mengi yanauza Vifaranga. Kuna bei tofauti tofauti sh 1300 . sh 1400. Sh 1500.
Kwahapa tuna tumia Vifaranga wa bei ya sh 1400
Utanunua kifaranga kimoja 1400×100=140000
Siku umeenda kuchukua sasa unatakiwa huku nyuma uwe umekamilisha yafuatayo,
Banda umelisafisha vizuuri, na unatenga kona moja ambayo utaitengenezea umbo la nusu duara  (brooder) ndani ya brooder kutakuwa  maranda pia weka magazeti , magazeti husaidia maji ya kimwagika utaweza kusafisha kiurahisi.
Bila kusahau vyombo vya chakula na maji  , chanzo cha joto unaweza tumia jiko la mkaa, balbu . chungu au taa ya chemli.
MATUMIZI KATIKA CHAKULA .
Vifaranga 100 kwa wiki 4 au 5 unaweza tumia mifuko 5 ya kg 50 mpaka kuuzwa.
Wiki Mbili za mwanzo🌀
Starter mash mfuko mmoja sh 60000 kwa mifuko miwili . 60000×2=
Sh 120000=
Wiki ya Tatu.🌀
Growers pellet   mfuko mmoja  73,000/=.
Wiki ya 4🌀
Finisher mash     57,000/= 57000×2=114000.
Jumla ✅
 Sh 114000+73000+120000+140000=
Sh 447000
Madawa na kununua maranda inaweza gharimu sh 53000.
Kwahiyo kwa matunzo hadi kuuzwa watagharimu sh 500000.
Katika kuuza kuku mmoja sh 6000 × 100=  Sh600000.
Faida ni sh 100000 kwa mwezi mmoja. ⚡
 utakavyo endelea kufuga  mtaji wako utaongezeka. Na utazidi kuwa mzoefu katika ufugaji wa kuku broiler. Pia bei ya chakula hutofautiana hii bei niliotumia ni hii baada ya chakula kupanda ila kuna sehemu chakula mfuko wa kg 50 inafika hadi sh 51000_54000..
Pia sio utasimamisha shughuli zako zote kwa ajili ya kuku.
Vitu vya kuzingatia kabla ya kuanza kufuga, chunguza kwanza soko lao lipoje kwahapo ulipo ili utakavyo wafuga kwenye kuuza wasije wakasumbua.
PITIA
SABABU ZINAZOWEZA KUATHIRI CHANJO

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

Njoo ujifunze kilimo cha nyanya

NYANYA ni zao linalopendwa kutumiwa….kunogesha chakula, chakula kilichowekwa NYANYA huwa na radha nzuri inayomvutia mlaji Wakulima wengi hutamani kulima zao hili wengi huandika FAIDA na

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »