Umwagiliaji wa Matone

Share on facebook
Share on whatsapp
Share on twitter
Share on telegram
Soma kwa umakini itakuchukua dakika chini ya Kumi......

Umwagiliaji wa matone ni mfumo wa kisasa kwa umwagiliaji wa mimea na hasa mazao. Maji hupelekwa polepole kwa mabomba au mipira yenye matundu madogo moja kwa moja hadi mguu wa kila mmea, karibu na mizizi yake. Mfumo huu unapunguza sana matumizi ya maji na pia shida nyingine mbalimbali.[1][2]

Vyanzo vya mfumo huu vinajulikana kutoka China ya Kale ambako wakulima walizika sufuria za kauri katika ardhi karibu na miti na kuizijaza maji, Maji yalipita kwenye kuta za vyombo na kuingia udongo karibu na mizizi polepole. Wajerumani walitumia mabomba ya udongo wa ufinyanzi uliochumwa ndani ya ardhi kwa umwagiliaji kuanzia karne ya 19. Baada vita kuu ya pili ya dunia mtu wa Australia alianza kutumia mabomba ya plastiki yenye matundu.

Ilionekana ya kwamba mbinu huu ni rahisi lakini una hasara kama mpira ni ndefu. Matundu karibu na chanzo cha maji hutoa maji zaidi kuliko matundu ya mbali. Pia kama shinikizo katika mpira ni juu kidogo maji hayatokei kwa umbo la matone mbali kwa nguvu mno kama mwendo mfululizo. Mfumo huu uliboreshwa nchini Israeli na Simcha Bass aliyeongeza nozeli za kutonesha maji (ing. dripper au emitter). [3]

Katika maeneo ya joto kubwa mfumo wote hupelekwa chini ya uso wa ardhi kwa kupunguza tena upotevu kutokana na usimbishaji wa maji hewani.

Faida za umwagiliaji wa matoneEdit

Faida za umwagiliaji wa matone ni kama zifuatazo:
◾Matumizi ya maji ni kidogo
◾Mbolea wa chumvi unaweza kuongezwa katika maji na kufikishwa karibu na mizizi pekee, hivyo matumizi yake yapungua pia
◾Maji yapelekwa pale amboka mimea inayahitaji, siyo pale ambako haihitajiki
◾Magugu yanapungua kwa sababu hayamwagiliwi (isipokuwa sehemu iliyo karibu sana na mazao)
◾Hatari ya magonjwa wa fungus inapungua kwa sababu majani yanabaki makavu
◾mfumo unahitaji shinikizo kidogo tu na hii inapunguza gharama za nishati (diseli, umeme) kwa ajili ya pampu
◾hata pampu ni ndogo hivyo rahisi zaidi
◾Mmomonyoko wa ardhi shambani unapungua sana
◾Hatari ya kuongezeka kwa chumvi ardhini inapungua sana

PITIA
Kitambue Kilimo cha Kahawa
Diana Mussa

Diana Mussa

Mwana Blogger mahiri,aliyehama fani yake kutoka kwenye urembo na mitindo hadi kwenye uwanda wa kilimo ,na kuitumia sekta hii ya kilimo kwa kutoa taarifa zilizo sheheni mambo tele ~ na kushare kwa Watanzania,katika ulimwengu huu wa Teknolojia

Leave a Reply {Acha Maoni yako hapa}

Kuhusu Sisi

KilimoTanzania tumejikita kukupa Elimu pekee ya Kilimo kwa Gharama sawa na Bure, Ili tuweze kuwa na Taifa bora lenye wajisiriamali katika sekta ya kilimo na Ufugaji.

Kwa Mawasiliano usisite Kubonyeza hapa 

Vitabu Vya Kilimo na Ufugaji pia vinapatikana  Kwe Ukurasa Huu

Jiunge channel Yetu ya Telegram

Karibu uweze Kujiunga na Channel Yetu ya Telegram uwe wa Kwanza kupata ,Taarifa moya za kuhusu Kilimo mara zinapowekwa kwenye Tovuti Yetu

Nyaraka Mpya

Follow Us

Video Mbali mbali za Kilimo