USTAWISHAJI WA TIKITI MAJI

USTAWISHAJI WA TIKITI MAJI
USTAWISHAJI WA TIKITI MAJI

USTAWISHAJI WA TIKITI MAJI : Zao la tikiti maji (Watermelon) asili yake ni Afrika na kwa sasa zao hili linalimwa sana Afrika
Magharibi na Mashariki, India, Indonesia na katika visiwa vya Caribbean. Aina za matikiti maji zinazofahamika ni Tomo Waston, Dixie Queen, Charleston Grey, Congo na Florida Giant.

USTAWISHAJI: Zao hili hustawi toka usawa wa bahari hadi meta 1000. Huvumilia aina tofauti za hewa na huhitaji unyevu wa kutosha katika hatua za mwanzo mradi tu upungue kadri inavyokaribia kukomaa. Unyevunyevu ukizidi sana husababisha magonjwa na hupunguza kasi ya utoaji wa maua. Pia joto kali hudhuru matunda.

KUPANDA: Mbegu hupandwa nyakati za mvua na matunda huvunwa nyakati za kiangazi. Hupendelea ardhi yenye rutuba, utifutifu na usiotuamisha maji. Mbolea ya takataka au samadi ndiyo ifaayo zaidi kwa sababu mbolea za chumvichumvi ni ghali mno kwa zao hili.

Mbegu hupandwa katika matuta au vilima vya udongo. Weka mbegu mbili au tatu katika kila shimo, baadaye ng’oa na kubakiza mche mmoja ulio na afya. Umbali kati ya mche na mche ni sentimita 180 kati ya mstari.

Ni muhimu kupalilia na kurudishia udongo kwenye mashina ya mimea. Nyakati za ukame, unyweshaji ni lazima. Pia inapendekezwa kutandaza nyasi kwa kuzungushia mashina kusudi kuzuia mizizi isidhuriwe na jua.

Katika hatua fulani ya kukua, inapendekezwa kubinya au kukata ncha za mimea jambo ambalo linasababisha kutoka kwa matawi mengi pembeni, ambayo hatimaye hubeba matunda.

Matunda huwa tayari kuvunwa baada ya majuma 12 hadi 15 tangu kupandwa. Matunda huliwa mabichi. Mbegu zilizokomaa huwa na mafuta na watu wengi huzikaanga na kuzitafuna.

PITIA
Kilimo cha Kunde

MAGONJWA:

Magonjwa ya zao hili ni sawa na yale ambayo hushambulia matango, yaani Cucumber Mosaic, Bacteria Wilt, Downy Mildew na Powder mildew.

Ugonjwa wa Cucumber Mosaic husababishwa na sumu ya virusi ambayo ni mbaya sana kwa zao hili. Hutoa madoa kwenye matawi na kufanya sura yake kuwa mbaya na wakati mwingine rangi ya matunda ya kijani kibichi hutoweka kabisa. Hali ikiwa mbaya zaidi mmea hugeuka njano, hudumaa na kushindwa kutoa matunda. Ugonjwa huu huenezwa na wadudu kama aphids na beetles. Njia za kukabiliana nao ni kufanya usafi wa bustani na kandoni mwake, kuangamiza wadudu wauenezao, kuharibu mimea iliyoshambuliwa na kupanda aina zinazovumilia ugonjwa huu.

Downy Mildew ni ukungu ambao huharibu matikiti na hasa nyakati za mvua na joto la kadiri husababisha madoa membamba na meupe au njano kwenye majani na matokeo yake ni kutoa matunda machache na duni. Ugonjwa huu hutibiwa kwa kunyunyiza dawa ya Copper au Zineb kila baada ya siku 10 na vilevile chimbia chini masalio ya mmea yaliyopatwa ugonjwa huu.

Powder Mildew ni ukungu ambao hushambulia majani na mashina ya mmea. Kwanza hutokea madoa madogo na meupe kisha husambaa kwenye mmea wote. Hatimaye rangi ya majani hufifia na mmea kufa. Ugonjwa huu hutibiwa na unga wa salfa kila baada ya siku 10.

WADUDU:

Cucumber Beetle mdudu huyu hushambulia miche ya zao hili mara inapochipua pia hushambulia majani ya mimea michanga. Njia ya kukabiliana na mdudu huyu ni kutumia dawa kama Rotane na Crylite kwenye miche michanga na kurudia kila baada ya juma moja.

Melon Aphids – mdudu huyu hufyonza utomvu wa mimea na kushambulia sehemu za chini za majani ambayo baadaye hukunjana. Huweza kudhibitiwa kwa kutumia dawa ya maji ya unga ya Malathion au Nicotine . Hakikisha dawa inafi ka upande wa chini wa majani.

PITIA
Ujue Muhogo

Pickle Worm – hushambulia sana matikiti, buu au funza hujipenyeza ndani ya ua au kitumba cha mmea, mwishowe huhamia kwenye tunda, mafunza mengine hutoboa mashina na kuishi ndani yake, lakini madhara zaidi hufanywa kwenye tunda. Njia ya kukabiliana nao ni kukusanya na kuchoma mimea na masalio yote yaliyokwisha ambukizwa na kunyunyizia dawa ya Rotane na Crylite kila baada ya juma moja.

FAIDA ZA TIKITI MAJI

Tunda hili lina wingi wa vitamin A na C ambazo ni muhimu kwa kusaidia macho yote kufanya kazi vizuri na kufanya ngozi zetu kuwa nyororo na imara kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

TIKITI MAJI TEYARI KWA KULIWA
TIKITI MAJI TEYARI KWA KULIWA

Hivi karibuni makala moja katika mtandao iitwayo Web MD ilimnukuu Dr. Bhim Patil ambaye ni mkurugenzi na mtafiti wa kituo cha uboreshaji wa matunda na mbogamboga katika chuo kikuu cha Texas Marekani akilitaja tikiti maji kuwa na kirutubishi cha protini kijulikanacho kama citrulline kinacho changamsha mishipa ya damu na kuitanua kama ifanyavyo viagra na hivyo kuweza kutibu matatizo ya ukosefu wa nguvu za kiume.

Alipoulizwa ni idadi gani ya matikiti maji mtu anapaswa kula ili kuongeza nguvu hakuweza kujibu moja kwa moja isipokuwa alisema mtu akiweza kula matunda haya 10 kwa kipindi fulani ataweza kupata miligramu 150 za citruline . Hata hivyo hakuweza kuthibitisha moja kwa
moja kama kiasi hicho kinaweza kutosha kutoa tiba hiyo.

Mtaalamu mwingine Daktari Irwin Goldsten ambaye ni mhariri mkuu wa jarida la “The Journal of Sexual Medicine’ anasisitiza wanaume kutumia sana matikiti maji ili kuongeza uwezekano wa kuboresha nguvu zao za kiume. Hivyo ni wakati wa mimi na wewe kuzithibitisha tafiti hizi kwa kutumia matikiti maji kwa wingi.

PITIA
Nyanya zinahitaji matunzo ili upate mavuno
JUISI YA TIKITI MAJI
JUISI YA TIKITI MAJI

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

Kitambue Kilimo cha Kahawa

UTANGULIZI Kahawa ni miongoni mwa mazao ya biashara ya biashara yanayoliingizia taifa mapato mengi, kahawa ni zao la pili la biashara baada Tumbaku. Asili:kwa mujibu

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »