WAJUE KUKU WENYE FAIDA

kuna mambo kadhaa ya kuzingatia kabla ya kuchagua aina bora ya kuku wa kufuga ili ikuletee faida uliyodhamiria. Ufugaji unaweza kukutengenezea kipato cha ziada au kukupa ajira ya kudumu kama utazingatia yafuatayo.

1. GHARAMAgharama zitakuongoza kufanya uchaguzi.kuku wa kisasa ni gharama sana.pia wanahitaji usimamizi wa hali ya juu,lishe kamili na bora ilikuwawezesha kuzalishavizuri na kwa ufanisi.kuku wa kienyeji/asili wana gharama ndogo na rahisi kuzoea mazingira ya huku kwetu.
wakipata matunzo bora wanaweza kuboresha uzalishaji.hata hivyo ukitaka kufuga idadikubwa na kutumia mlo kamili(balance diet),ni vyema kuchagua kuku chotara(hybrid).      
2.HALI HALISI YA SOKOni muhimu sana kuzingatia hali halisi au uhitaji wa soko lililokuzunguka.kama soko lipo la kuridhisha chagua kuku chotara wenye uzito wa wastani.kama mayai na nyama vinatoka na pia upatikanaj wa mlo kamili     (kuku wa kahawia) ni wa uhakika.
kama unataka kuuza mayai,zingatia jamii ya kuku wepesi (light breed) kuku wale weupe wa mayai.mazingira mengine tofauti na hapo chagua jamii ya kuku wazito(heavier) mara nyingi wale wa kahawia (brown layers)  ndio chaguo linalostahili.kama unaishi maeneo ya mbali na soko na unataka kuzalisha mayai kwa matumizi ya nyumbani,na kuuza mayai ya ziada na nyama kwenye eneo ulilopo,hapo chagua kuku wa asili/kienyeji.


 3.UZOEFUkuna msemo unasema “experience is the best teacher” mwalimu mzuri n uzoefu,kama huna uzoefu hata kidogo ni vyema ukaanza kwa kufuga kuku wa asili ambao ni wa gharama nafuu.
4.USIMAMIZI WA MRADI/BANDAkama usimamizi wa banda au mradi wako ni mzuri,anza kufuga kuku wa kisasa ambao wanafaida kubwa usimamizi mbovu ni sababu mojawapo ya kushindwa kufanya vizuri kwa miradi mingi na hivyo kupelekea kufungwa.usimamizi kwenye :usafi,kulisha kiasi sahihi na kwa muda muafaka,kutoa taarifa haraka,utunzaji kumbukumbu na mengineyo.
5.MAPENDEKEZO YA WENYEJIinategemea na maeneo,sehemu nyingine hasa mjini,watu hupendelea mayai ya kahawia au yenye kiini cha njano,wengine wanapendelea mayai ya rangi nyeupe.kumbuka “mteja ni mfalme”.
 6.UPATIKANAJI WA MBEGU ZA KUKU KIURAHISIkuku hawa wa kisasa mara nyingi huwa hawapatikani kwa urahisi,inategemea na upatikanaji katika eneo husika.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

MISINGI YA KILIMO BORA CHA BINZARI

na la kitalaam ni Curcuma domestica au Curcuma longa na kwa kiingereza niturmeric. Zao hili asili yake ni Mashariki ya Mbali, na linalimwa zaidi katika mkoa wa Tanga, Kagera,

Read More »

Kilimo cha Kabichi

Unaweza kulima kabichi msimu wote wa mwaka. Soko lake ni la uhakika katika kipindi chote na ni muhimu kwa afya. Pia, linaweza kutumika kama malisho

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »