YAFAHAMU MAGONJWA , WADUDU WANAOTHIRI KILIMO CHA PILIPILI MBUZI NA JINSI YA KUEPUKA

Magonjwa.

1. Fusarium wilt (Mnyauko)Njinsi ya kuepuka. .Tandika shamba lako na majani makavu ili kupunguza joto.
•Ng’oa mimea yote iliyougua na choma moto mabaki.
•Epuka kusambaza ugonjwa kwa kusafisha vizur vifaa vya shamba na chini ya miguu uingiapo shambani.•Jitahidi mimea iwe na afya nzuri kwa kuweka mbolea na maji ya kutosha.•Pulizia dawa ya fangas kama vile ortiva.

2) Southern blight ( Sclerotium wilt)
Huu ungonjwa utaona kwenye shina china panaota fangasi weupeweupe (Whitish fungal growth on the stems of infected plant) .Majani ya chini huweza kunyauka,Huu ungonjwa hutokea muda mfupi kipindi cha joto kali.Kuepuka/Kuzuia.
•Wakati wa kulima ..lima hadi chini sana ili hao fangasi waende chini sana ambapo mizizi haifiki.
•Mimea iliyoshambuliwa…Ing’oe yote na choma moto lakini chomea nje ya eneo la shamba.•Pulizia Ortiva.

3) Anthracnose.
Huu ni ugonjwa wa kawaida kwenye pilipili mbuzi na huu ugonjwa huweza kukaa ardhini muda mrefu.Dalili zake utaona matunda kama kuna sehemu zinakuwa nyeusi na panajaa majimaji …dalili hii huenea sehemu kubwa ya tunda na baadaye tunda huoza.

Kuepuka.
Kuepuka ugonjwa kujirudia musimu na musimu..Baada ya kuvuna choma mabaki yote.•Shamba ambalo ulilima pilipili usirudie kulima pilipili mfululizo zaidi ya mara mbili…badilisha zao kwa kupanda zao ambalo sio jamii moja na pilipili mbuzi (Do crop rotation).•Pia huu ugonjwa huweza kupitia mbegu…kwa hiyo mkulima lazima achukue mbegu kutoka kwa wakala aliyeidhinishwa na mwaminifu…mbegu hazitakiwi kutengenezwa kutoka kwenye mimea iliyoathirika na ugonjwa.

4) Bacteria.
Madoamadoa ya bacteria kwenye matunda….huweza kutokea na kusambaa haraka wakati wa joto kali na unyevu kwenye udongo.Pia huu ugonjwa huweza kuenea kupitia mbegu.

PITIA
MKULIMA NUFAIKA KWA KILIMO BORA CHA MIWA

Dalili zake utaona madoamadoa ya kama brown chini ya majini na pia kwenye matunda.Kuepuka.
•Usitengeneze mbegu kutoka kwa mimea iliyoathirika na huu ugonjwa.Nunua kutoka kwa wakala.•Pulizia dawa yoyote copper.

5) Virusi.
Kuna aina nyingi ya virusi ambao hushambulia pilipili mbuzi.Dalili zake ni majani kuwe ba njano na kujikunja .

Kuepuka.•Nunua mbegu bora•Pulizia dawa za wadudu kuanzia kwenye kitaru na kuendelea.Wadudu wanaosababisha virus sanasana na wadudu mafuta (Aphids) kwa hiyo akikisha muda wote shambani hakuna hao wadudu kwa kupulizia Actara.NB:Pamoja na maelezo yote hapo juu.Usikae zaid ya siku 14 bila kupiga dawa ya wadudu na ukungu/fangasi hata kama hakuna ugonjwa.
Wadudu.
Pilipili mbuzi hushambuliwa na ;

1. Wadudu mafuta ( Aphids)Kuwadhibiti.Tumia Actara 8g/20L.Au tumia wadudu wanaokula wadudu mafuta,mfano special beetles.
2. Crickets
Hawa wadudu hukaa aridhini karibu na mmea na usiku hutoka walipo jificha na kukata miche michanga.Kawadhibiti.
Unapo andaa shamba andaa vizur ili nyumba zao zife na kuwaacha katka halu ya hatari ya kuliwa na ndege na wadudu wengine ,kama ni miche na iko kwenye tray…basi weka hizo tray juu ya kichanja.

3. Beetle.
Tuma Karate 40cm/20L.

4. Utitiri
Dawa:Tumia Dynamec au yoyote yenye Abamectin.

5. Nematodes 
Tumia solvigo.

Mavuno.
Pilipili huwa tayari kwa kuvunwa siku 60 hadi 95 kutegemea na aina ya mbegu uliyotumia. Chuma kwa uangalifu bila kung’oa mmea ili uendelee kuzalisha. Muvuno yanaweza kudumu kwa muda wa mwezi 1 hadi 3.

Usalama wakati wa uvunaji.
Pilipili huwa na kemikali iitwayo capsaicinoids ambayo inaweza
kukuwasha kwenye ngozi au kwenye macho ikiwa utajigusa. Vaa gloves wakati wa kuvuna na kuwa mwangalifu usijiguse kwenye macho.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

Mpunga / mchele

KILIMO BORA CHA MPUNGA

Mpunga ni kati ya mazao ambayo yanalimwa sana dunian na pia ni kati ya mazao ambayo yanapendwa sana na watu kutokana na chakula chake kuwa

Read More »

KILIMO BORA CHA KOROSHO

Korosho ni zao ambalo chimbuko lake ni Portuguese na baadae 16 century ndipo lilipo fika africa katika nchi ya msumbiji na baadae likafika nchini Kenya

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »