YAFAHAMU MAGONJWA YA KUKU KIUNDANI ZAIDI NA JINSI YA KUYATIBU.

Siku ya leo tutaendelea na kwa kuangalia magonjwa mengine  ya kuku ambayo hutibika kwa dawa kama ifuatayo:
 1.KUHARA DAMU (coccidiosis) Ugonjwa huu husababishwa na virusi.
Dalili.

 • Kuku huzubaa na kujikunyata
 • Kuku kuharisha kinyesi chenye damu au kinyesi cha kahawia
 • Kuku hudhoofika,manyoya huvurugika na kulegea mabawa na kuonekana kama wawevaa koti
 • Kuku hupungukiwa homa ya kula
 • Vifo huwa vingi kwa vifaranga

Tiba ya ugonjwa huu.Wape kuku wako dawa kama Esb 3, Amprolium, au Basulfa.

Kinga za ugonjwa huu.Zingatia usafi wa banda la kuku na usiruhusu unyevuunyevu katika banda la kuku.
2. HOMA YA MATUMBO(Fowl typhoid)
        Husababishwa na bakteria

Dalili za ugonjwa huu ni;

 •  Kuku hupata homa kali
 •    Kuku huarisha kinyesi cha kijani au njano
 •    Vifo huwa vingi hasa kwa vifaranga wenye wiki 1-2
 •    Kuku huzubaa,kuvimba viungo vya miguu,kuchechemea,kukosa hamu ya kula
 •    Kuku wanaotaga hupunguza utagaji,hutaga mayai yenye ganda laini na hupata   vifo vya ghafla

Tiba za ugonjwa huu.
  Dawa za oxytetracycline kama Furamax,Typhoprim hutibu ugonjwa huu.

Kinga za ugonjwa huu.
  Hakikisha usafi wa banda na vyombo vya chakula na maji kwa kuku.
  Tenganisha kuku wagonjwa na wazima

3. MINYOO
Hushambulia kuku wote wakubwa na vifaranga

Dalili za ugonjwa huu

 • Kuku hukonda
 • Kuku huarisha
 • Kuku hukohoa
 • Kuku hupunguza utagaji
 • Kuku hudumaa katika ukuaji/hawakui vizuri
 • Kuku hupungua uzito

Tiba za ugonjwa huu.
Tumia dawa za minyoo kama piperazine

Kinga za ugonjwa huu.Wapewe dawa za minyoo mara kwa mara kila baada ya miezi mitatu

4.VIROBOTO/CHAWA/UTITIRI
   Hushambulia sana vifaranga na hutokea vifo kwa wingi kwa vifaranga Kwa kuku wakubwa tatizo halionekani kwa sana lakini nao huathiriwa sana.

PITIA
NJIA SAHIHI ZA KUTUNZA MAYAI YA KUKU

Dalili za ugonjwa huu.

 •  Kuku kutochangamka
 •  Ukuaji mdogo wa kuku
 •  Kuku kutotaga na kuhatamia vizuri kutokana na kusumbuliwa na chawa,utitiri au  viroboto
 •  Viroboto huonekana kuganda machoni wakinyonya damu

Tiba za ugonjwa huu
Tumia dawa za unga kama sevin dust 5% ,Malathion ,akheri powder kwa kuku wote na mabanda yao.

Kinga za ugonjwa huu.

 Boresha usafi wa mabanda ya kuku.

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

KILIMO BORA CHA MAPAPAI

KILIMO CHA MIPAPAI •Kwa jina la kisanyansi ni Carica papaya,jina la kawaida ni papai. •Tunda la mpapai lina virutubisho vya vitamin A,B na C kwa

Read More »

KILIMO BORA CHA SOYA

Soya ni zao jamii ya mikunde ambayo ina baadhi ya sifa za mbegu zinazozalisha mafuta. Zao la soya lina protini nyingi yenye ubora wa hali ya

Read More »

KILIMO BORA CHA ULEZI

Ulezi ni punje ya mlezi au mwele (aina ya nafaka) ambao hulimwa katika sehemu zenye hali ya ukame. Ulezi ni zao la asili, shirika la

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »