Zao la Muhogo Laongeza Ufaulu kwa Wanafunzi Handeni

Kilimo cha zao la muhogo kimeongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi na kipato kwa wakulima wilayani handeni Akiongea na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wakati wa ziara ya kutembelea wakulima wa muhogo mkoani Tanga Mkurugenzi Mtendaji wa Malmashauri ya wilaya ya Handeni Bwana William Mkufwe amesema kabla ya kuanzisha programu ya kuendeleza zao la muhogo wilayani hapo wanachi wengi walikuwa na kipato kidogo pia hali ya upatikanaji wa chakula haikuwa nzuri hivyo kuathiri ufaulu wa wanafunzi mashuleni . Anasema kuwa Halmashauri walikubaliana kusimamia mpango wa kila kaya kuwa na ekari moja ya zao la muhogo na na kutumia mashule kulima na kusambaza mbegu kwa kaya mbalimbali lengo likiwa ni kuimarisha upatikaji na usambazi wa mbegu bora ambapo utekelezaji wake ulikuwa na majibu chanya kwa kiasi kikubwa. Kutokana na mavuno yaliyopatikana mashule yalianza kutoa chakula kwa wanafunzi hivyo kusababisha kiwango cha taaluma kuongezeka, akitolea mfano katika halmashauri yake amesema katika matokeo ya darasa la saba 2017 kiwango cha ufaulu kiliongezeka kutoka asilimia 61 mwaka 2016 mpaka 73 mwaka 2017, kidato cha pili kiwango cha ufaulu ili kiliongezeka kutoka asilimia 87 mwaka 2016 mpaka asilimia 91 mwaka 2017 na kidaoto cha nne kiwango cha ufaulu kiliongezeka kutoka asilimia 66 mwaka 2016 mpaka asilimia 76 mwaka 2017alisistiza bwana Mkufwe. Akiendelea kueleza matokeo chanya ya muhogo wilayani humo Mkurungezi anasema katika Tarafa za Kwa Msisi na Kwa Sanga muitikio umekuwa mkubwa ambapo zao la muhogo limestawi na kila kaya wameweza kulima zaidi ya ekari tano na zimestawi vizuri sana. Aidha katika upatikanaji wa soko bado kuna changamoto kidogo japo mikoa ya jirani kama Morogoro na Dar es salaam wanategemea wilaya ya Handeni kwa kiasi kikubwa sana Naye mkuu wa wilaya hiyo Bwana Godwin Gondwe anasema kuwa wilaya imekuwa ikiendelea kuwasiliana na na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kusaidia upatikanaji wa mbegu za kutosha wakulima wote wilayani humo. Anasema kituo cha Utafiti cha Kilimo cha Mikocheni kimekuwa mstari wa mbele katika kuipatia wilaya hiyo mbegu za muhogo na kituo hicho kimeahidi kutoa mbegu 400 kwa wakulima ambao hawakuweza kupata mbegu bora za muhogo. Aidha shirika la world vision limeendelea kuunga mkono uimarishwaji wa zao la muhogo nchini kwa kuchangia kiasi cha fedha shilingi milioni 60 kwa ajili ya upatikanaji wa mbegu za muhogo wilayani hapo ambapo zilisaidia upatikanaji na wa mbegu alisema Bwana Gondwe. Katika kutatua changamoto ya masoko ya zao hilo Mkuu wa Wilaya hiyo amesema kuwa wameshatenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa uwekezaji wa viwanda vya kusindika zao hilo na taratibu zinaendelea ili kuweza kulipata soko la china ambalo itifaki ilisainiwa siku kadhaa zilizopita. Kuluthum Rashidi Mdoe ni mkulima wa muhogo wa kijiji cha Kwa msisi wilayani handeni anasema msimu huu ni wa pili ambapo mwanzo alilima eka tatu za muhogo na akaweza kumlipia karo ya shule mtoto wake anayesoma shule ya binafsi na ameweza kununua pikipiki , jokofu na sasa ameanzisha biashara ndondogo. “Msimu uliopita niweza kupta milini 3.7 baada ya kuuza kwa jumla mihogo yangu nikanunua jokofu sasa natengeza barafu,nimlipa karo ya shule mwanangu anasoma Tanga mjini na nimenunua pikipiki. Sasa nini eka nane na nategemea kuanza kuvuna mwezi wa tano mwaka huu nategemea kujenga nyumba ya kupangisha.alisema Kuluthumu Naye Mohamedi Saidi mkulima kutoka kijiji cha kwa Msisi anasema msimu huu sasa analima ekari 15 wakati msimu uliopita alilima ekari mbili ambazo zilikuwa ni mbegu hivyo aliuza mbegu kwa wakulima wengine na mihogo aliweza kuuza kwa wachuuzi

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

KILIMO CHA UYOGA

Kwa kuwa #uyoga upo wa aina mbalimbali, usitawishaji wake hutofautiana katika mahitaji yake, ikiwa ni pamoja na hali ya hewa, malighafi za #kuoteshea, urahisi wa

Read More »

CORONA VIRUS EDUCATIONAL POST

Naomba twende polepole Vyanzo vya vifo duniani na idadi (WHO, 2019) Heart diseases – mil 9.43Stroke – mil 5.73COPD – mil 3.04Pumu – mil 2.96Alzheimer’s

Read More »

Kilimo Bora cha Mahindi

MWONGOZOWA KILIMO BORA CHA MAHINDI ABDUL A. MKONO (MWL ABUU), Bsch AEA, SUA Engineer OCTAVIAN J LASWAY BSc Irrigation and water resources (SUA) UTANGULIZI Mahindi

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »