ZIFAHAMU AINA NNE ZA MTAMA

Mtama ni kundi la mbegu punje ndogo katika jamii ya nafaka ambayo ina kiasi kikubwa cha kabohaidreti.Ni zao lenye uwezo mkubwa wa kuvumilia hali ya ukame kuliko mazao mengi ya jamii yake,Hivyo hulimwa maeneo mengi Duniani yenye mvua Pungufu na hata yenye mvua za kutosha.Ni moja ya zao ambalo likitumika vizuri husaidia kwa kiasi kikubwa kukabliana na mabadiliko ya hali ya nchi na pia katika vita ya kuzuia njaa.Mtama hutumika Kama vile unga wa ugali,kupikia mikate ya mtama,kupika ubwabwa wa mtama,Unaweza kuchemshwa na Kuliwa (mnyoma-lugha ya kiasili),Viwanda vya bia kutengeneza bia,Pia majani na mabua yake yanaweza kutumika kama chakula cha mifugo,na pia mabua Makavu yanaweza kutumika katika kujengaea uwa .

HALI YA HEWA IFAAYOMtama ni zao linaloweza kustahimili ukame.Hivyo unaweza kulimwa na kukua kuanzia ukanda wa chini wa bahari 0 – 100 mita hadi Mwinuko wa mita 1500.pia unaweza kulima zaidi ya hapo lakini pasiwe na baridi kali mtama haukubali seheme zenye baridi.Huitaji kiasi cha mvua cha wastani wa milimita 300 – 800 za kwa mwaka ili uweze kukua vizuri.Mtama hukubali sehemu zenye joto hivyo huitaji nyuzi joto 18 – 33 °C.

ARDHI IFAAYO KWA KILIMO CHA MTAMAMtama unapenda ardhi ambayo haituamisdhi maji na mwingine unavumila katika ardhi inayotuamisha maji kidogo,hivyo kwa mavuno mazuri usipande katika ardhi ambayo hutuamisha maji kwa ajili ya kupata mavuno bora,kama ni udongo wa mfinyanzi hakikisha maji hayasimami shambani kwa muda mrefu ikinyesha mvua.Mtama hukubali katika kichanga chenye rutuba au mchanganyiko wa mchanga na mfinyanzi au mfinyanzi.Hukua vizuri katika udongo wenye soil PH 5 – 9.

PITIA
Umuhimu wa kitunguu swaumu katika kutibu magonjwa ya kuku

MAANDALIZI YA SHAMBAAndaa shamba lako mapema kabla ya msimu wa kupanda mtama kuanza.Shamba lisafishwe na kulima kwa jembe la mkono,jembe la kukokotwa na Ng’ombe au trekta na pia unaweza kupanda bila kulima (zero tillage).

MBEGU BORA ZA MTAMAZipo aina mbalimbali za mtama na mbegu zake.Aina hizi hutofautiana kulingana na rangi zake,nyekundu,kahawia,nyeupe ambazo zinajumuisha aina zaidi ya 20 za mtama duniani.Pia mtama na aina zake huwa kuna ambao ni mtama mchachu (Hasa mbegu za kahawia na nyekundu),mtamu hasa Rangi nyeupe.Wakulima wengi hupendelea mtama mweupe.Pia mtama wa mbegu sa kisasa huwa laini kuliko mbegu za asili ambao ni mtama mgumu.Mtama wa asili huwa ni mbegu ndefu kwenda juu na huchukua muda mrefu kupanda hadi kuvuna kuliko mtama wa kisasa ambao mwingi ni mfupi na huchukua muda mfupi zaidi na hutoa mavuno bora zaidi ya mtama wa asili.

AINA HIZO NI KAMA VILE;1.SEREDOHii ni aina nyingine yenye punje za kahawia, na inapendekezwa Kulimwa kwenye eneo lenye mwinuko wa mita 1,500 kutoka usawa wa bahari. Aina hii huchanua baada ya siku 71 na hukomaa katika kipindi cha siku 120. Aina hii huwa ni ndefu, na ina uwezo wa kuzalisha Tani 2 kwa ekari moja. Ina uwezo wa kukabiliana na ugonjwa wa milia, kutu, mabaka kwenye majani, na madoa ya kahawia kwenye majani.

2.SERENA na DOBBS.Aina hii huwana punje za kahawia. Aina hii hustawi kwenye eneo lenye mvua za wastani na hukomaa katika kipindi cha siku 110. Aina hii huwa na shina na mizizi imara, ambapo huweza kuzalisha kiasi cha Tani 1.5 kwa ekari moja. Ambapo zinahitajika kilo 5 za mbegu kwa hekari moja. Aina hii ina uwezo wa kukabiliana na ugonjwa milia, kutu, na madoa ya kahawia kwenye majani.


3.GADAMHufanya vizuri katika sehemu ambazo si kame sana. Katika nchi nyingi mfano Kenya, aina hii ya mtama hutumika kutengenezea bia na pia kwa chakula. Aina hii huvumilia bungo na ugonjwa wa majani.

PITIA
Hii ndio siri ya mbegu na ganda la tikiti maji kwa wapenzi

4.HAKIKA NA WAHIHizi ni aina mbili za mtama ambazo zimezalishwa na kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga kwa ajili ya kuoteshwa kwenye mashamba yalioathiriwa na viduha. Mbegu hizi zina rangi ya manjano iliyopauka. Unga wa aina zote mbili zinafaa sana kwa kupika ugali.

5.PATO na MACIAHizi hutoa mbegu nyeupe laini na hufaa kwa ugali na hata kwa unga wa Dona (kusaga bila Kukoboa)

6.MBEGU NYINGINETegemeo,Lulu,Sandala,Imani.

7.MBEGU ZA ASILI

Huchukua muda mrefu kupandwa hadi kuvunwa.Zaidi ya siku 120

Jiunge Nasi Telegram

Usipitwe na Nyaraka mpya kila zikiwekwa kwenye Tovuti yetu na weza kujifunza kwa kina ukitumia simu. Jiunge sasa hapa.

ZIJUE FAIDA ZA KULIMA MAPAPAI

Hili ni aina ya zao la matunda linalopatikana katika familia ya caricaceae na linajulikana kwa jina la kisayansi carica papayaPapai ni moja ya matunda ambayo huchukua

Read More »

Kilimo bora cha Mtama

UTANGULIZI Mtama ni miongoni mwa mazao ya nafaka yanayolimwa kwa wingi nchini na duniani kote. Zao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara. Mtama

Read More »

KILIMO BORA CHA MAPAPAI

KILIMO CHA MIPAPAI •Kwa jina la kisanyansi ni Carica papaya,jina la kawaida ni papai. •Tunda la mpapai lina virutubisho vya vitamin A,B na C kwa

Read More »

Kilimo cha Tufaa

Tufaa ni tunda moja maarufu duniani ambalo hupendwa kuliwa na watu wa jamii zote, hii inatokana na utamu wake pamoja na faida za kiafya zinazopatikana

Read More »

UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI

Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo

Read More »